Emmerson Mnangagwa: Avalia skafu inayobadilisha picha ya Zimbabwe

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akiwa amevalia skafu yenye rangi za bendera ya Zimbabwe Haki miliki ya picha AFP
Presentational white space

Mtindo mpya wa kuvalia skafu unamsaidia rais mpya wa taifa hilo kulipatia picha mpya taifa hilo-na kujitenga na mtangulizi wake Robert Mugabe na utawala wake wa miaka 37.

Tangu mkutano wa Davos mnamo mwezi Januari, Emmerson Mnangagwa amekuwa akivalia kitambaa hicho kilicho na rangi za bendera ya Zimbabwe katika shingo yake -bila kujali viwango vyovyote vya joto.

Skafu hiyo ilisaidia sana wakati wa hali ya baridi kali iliokuwa katika milima ya Uswizi- na rais huyo wa Zimbabwe alivalia skafu hiyo wakati wa mahojiano na BBC , na baadaye kutuma ujumbe katika mtandao wa twiter akisema kuwa , Zimbabwe iko wazi kwa biashara.

Lakini sasa kitambaa hicho kimekuwa kitu cha kawaida kwa Mnangagwa mbali na mkutano wa kiuchumi duniani wa World Economic Forum - na kina alama yake ya reli #EDscarf.

Raia huyo anayejulikana na herufi zake kama ED , alikipata kitmbaa hicho kwa bahati baada ya mama na mwanawe kuwasiliana na wizara ya maswala ya kigeni siku ya Jumamosi kabla ya ujumbe wa Zimbabwe kuondoka kuelekea mjini Davos.

'Kitu cha kushangaza'

Kulikuwa na hisia nyingi kabla ya mkutano huo na kiongozi mpya wa Zimbabwe alijitahidi kuvutia uwekezaji wa haraka ili kufufua uchumi ambao umekuwa umeshuka muongo mmoja uliopita

"Tulipiga simu na tukasema tuna hizi bidhaa , hatujui mutazitumia vipi .Ni kitu kilichofuatia 'unamuona rais amevalia skafu'' ...kilikuwa kitu cha kushangaza sana upande wetu, Celia Rukato aliambia kipindi cha habari cha BBC.

Alisema kuwa ilikuwa miongoni mwa bidhaa zake za kwanza ambazo yeye na mamake Hesphina Rukato walitengeza wakati walipoanzisha kampuni yao 2014, ziliuzwa zikiwa na umaarufu mdogo katika duka la kuuza vinyago la Harare katika uwanja wa ndege.

Ilikuwa njia ya raia wa Zimbabwe kuonyesha waliipenda sana Zimbabwe.

Walipendelea skafu iliokuwa katika alama ya reli ya #ThisFlag iliotumika na vuguvugu la 2016 lililopinga uongozi wa Mugabe na hali mbaya ya kiuchumi.

Skafu hiyo ilizinduliwa na muhubiri aliyekasirishwa na hali ya taifa hilo.

Alichapisha kanda ya video katika mtandao wa facebook ya yeye akiwa amejifunga bendera ya Zimbabwe, akielezea umuhimu wa rangi hizo.

''Wananiambia kwamba kijani ni ya ardhi, na mimea-sioni hata mmea mmoja katika taifa langu'', Evan Mwawarire alisema.

Manjano ni ya madini- sijui ni idadi gani ya madini ya almasi yaliosalia- sijui ni nani aliyeuziwa na mapato ni kiwanhgo gani cha mapato waliopata.

''Rangi nyekundu ni ya damu iliomwagika ili kujipatia uhuru kwa hilo nashukuru sana-Sijui iwapo walikuwa hapa wale waliomwaga damu yao-wakiona vile taifa hilo lilivyo watataka damu yao kurudishwa'',

Kabla ya Mugabe kuondolewa , wafanyibiashara wadogo wadogo walipigwa marufuku kutouza bendera bila ruhusa.

Lakini wakati wa maandamano , siku chache kabla ya Mugabe kujiuzulu , bendera ilikuwa kila mahali katika shingo za raia wengi wa Zimbabwe bila kujali tofauti ya vyama vyao.

'Vazi la kitaifa'

Kufuatia kuvaliwa vazi hilo la skafu katika mkutano wa Davos , imekuwa ni lazima sasa kwa wale wanaowakilisha taifa hilo ng'ambo kuvaa skafu hiyo

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii