Msaada kwa walio na ulemavu duniani

Halima ana miaka 25, ameketi mbele ya mashine yake ya kushona nguo Haki miliki ya picha UCEP Bangladesh
Image caption Halima ana miaka 25, ameketi mbele ya mashine yake ya kushona nguo

Watu wengi wenye ulemavu wa viungo katika nchi zilizo masikini duniani hawawezi kwenda shule au hata kutafuta kazi.Vikwazo kama vile unyanyapaa au kutopata usaidizi kunawafanya washindwe kutambua umuhimu wao kwenye jamii.

Miradi ya jamii inayopata usaidizi kutoka UK aid, inajaribu kuondoa changamoto hizi kwa kuwekeza na kuboresha, maisha ya watu wanaoishi na ulemavu

Kutana na watu ambao maisha yao yamebadilika kutokana na programu hizi.

Nchini Bangladesh, Halima mwenye miaka 25 alizaliwa akiwa hana mkono wa kushoto.Wazazi wake hawakumudu kumpeleka shule.

Lakini hatimaye alipata msaada kutoka shirika liitwalo UCEP Bangldesh, Halima akajifunza ushonaji wa nguo hasa umaliziaji na masuala yahusuyo ubora wa mavazi.kwa sasa ana kazi inayomuwezesha kupata dola 100 kwa mwezi.

Anasema, ''Nina furaha, imi si mzigo kwa mtu yeyote tena.Ninaweza hata kuwasaidia wazazi wangu''.

Ramesh, 18, alipoteza miguu yake wakati wa tetemeko la ardhi Nepal.Alipata msaada wa taasisi ya Humanity and Inclusion.Sasa anafundishwa kuwa mwanamichezo muogeleaji

Haki miliki ya picha Lucas Veuve / Humanity and Inclusion
Image caption Ramesh akiwa kando ya bwawa la kuogelea
Haki miliki ya picha Jo Harrison / DFID
Image caption Wanaume walemavu wakicheza mpira wa kikapu

Shaher alizikwa akiwa hai baada ya kupigwa risasi mgogoro wa Syria ulipoanza.Alidhaniwa kuwa amekufa.

Lakini binamu yake alipompata, aligundua kuwa alikuwa akipumua.Alimvuta nje na kumpeleka hospitali

Tangu wakati huo Shaher alikuwa akipata matibabu na akajiunga na timu ya wachezaji wa mpira wa kikapu walio katika viti vya magurudumu sambamba na raia wengine wa Syria waliokuwa wamejeruhiwa katika vita.

Haki miliki ya picha Jo Harrison / DFID
Image caption Wachezaji wakiwa uwanja wa mpira wa kikapu
Haki miliki ya picha Aurelie Marrier d’Unienville/Sightsavers
Image caption Sylivia akiwa amekaa kitandani kwake

Sylivia ameona ni namna gani maisha yanakuwa magumu ukiwa na ulemavu.Alipokuwa mlemavu wa kutoona, mume wake alianza kumuona mzigo .Baada ya unyanyasaji wa miaka adhaa, alilazimika kuondoka nyumbani.

Hivi sasa, Sylivia ana makazi mapya katika mji wa Masindi nchini Uganda, akiwa na kazi yake.Anafundisha wanafunzi wenye ulemavu ujuzi aliokuwa nao.Hii inawapa wanafunzi wake nafasi ya uweza kujisimamia wenyewe.

Kwa kufanya hivi anawasaidia wengine kuepuka magumu aiyoyapitia kwa miaka mingi.

Haki miliki ya picha Aurelie Marrier d’Unienville/Sightsavers
Image caption Julius akimbusu mkewe shavuni

Julius alipoteza uoni wake baada ya operesheni ambayo haikufanikiwa.Alifikiri asingeweza kumpata mpenzi mpaka pale alipokutana na mke wake Najiba, alipokuwa kwenye programu inayoendeshwa na taasisi ya misaada ya SightSavers.

Kwa sasa wana biashara kadhaa mjini Kampala, Uganda na wamebarikiwa watoto watatu.

Mbali na kuwa na duka la kuuza DVD na biashara ya ushonaji, wana shamba,kama unavyowaona hapo chini.Kwa sasa wana mpango wa kujenga kituo cha mafunzo kwa ajili ya watu wenye ulemavu jijini Kampala.

Haki miliki ya picha Aurelie Marrier d’Unienville/Sights
Image caption Julius na mkewe wakiwa shambani
Haki miliki ya picha Aurelie Marrier d’Unienville/Sightsavers
Image caption Simon Peter Otoyo akiwa nje ya nyumba yake

Simon Peter Otoyo ndio kwanza amerejea kutoka shuleni ambako waasi wa Chama cha Lord's Resistance Army (LRA) cha Joseph Kony walipofika kijijini kwake kaskazini mwa Uganda.

Walimfunga mikono yake yuma na wakamkata,samamba na kaka zake watatu.Akiwa mwanajeshi mtoto akikifanyia kazi kikosi cha LRA, Simon Peter akiwa na miaka 11 alipewa silaha na akapelekwa kwenda kupambana na jeshi la serikali.

Wakati wa vita kali mwaka 1996, risasi ilimjeruhi kichwani hali iliyoathiri jicho lake la kushoto na kumfanya kushindwa kuona tena.miaka kumi baadae,maisha yake yamebadilika , kwa sasa anapambana na mitazamo hasi dhidi ya ulemavu wa kutoona nchini Uganda.

Haki miliki ya picha Jeffrey DeKock / ICS
Image caption Mwanaume mmoja akimfundisha mtoto lugha ya ishara

Kikosi cha kujitolea cha British International Citizen Service (ICS) kiliweza kutumia miezi mitatu wakuwa wanafanya kazi na jamii ya watu wasioona kwenye kaunti ya Nandi,nchini Kenya ili kufundisha kuhusu haki za walemavu viziwi na kuboresha mahusiano kati ya jamii ya walio viziwi na wasio viziwi.

Jamii ya wasiosikia mjini Nandi mara nyingi inakabiliwa na unyanyapaa na kukosa msaada wanaouhitaji

Wanaojitolea walifanya kazi na mashirika mbalimbali ya kijamii kufundisha lugha za alama na kupanua uelewa wao kuhusu ule,avu wa kutosikia.

Walianzisha maandamano mjini Kapsabet.Mchanganyiko wa wasiosikia wakiwemo wanafunzi kutoka shule ya viziwa ya Kapsabet, wakitaka kuungwa mkoo zaidi katika kupata haki zao, na rasilimali za viziwi, ikiwemo elimu bora na nafasi za ajira

Haki miliki ya picha Jeffrey DeKock / ICS
Image caption Dickson Juma akiandamana katika siku ya uelewa kuhusu ulemavu wa kutosikia, Kapsabet, Kenya
Haki miliki ya picha Jeffrey DeKock / ICS
Image caption Elimu kuhusu ulemavu wa kutosikia iliandaliwa na Deafway ICS volunteers Kapsabet nchini Kenya

Mitandao inayohusiana

BBC haina haihusiki vyovyote na taarifa za mitandao ya kujitegemea