Zimbabwe: Mambo 10 yatakayokusaidia kufahamu yanayojiri Zimbabwe

Rais Robert Mugabe

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Rais Robert Mugabe

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe alijiuzulu mwishoni mwa mwaka baada ya kuwa madarakani kwa karibu miongo minne. Haya ni mambo 10 ambayo yatakufanya uelewe nchi hiyo imefikia wapi hivi sasa.

Rais mmoja ametawala tangu uhuru

Rais Mugabe aliyeongoza vuguvugu la kimapinduzi , amekuwa madarakani tangu nchi hiyo ilipojipatia uhuru mwaka 1980.Kwanza alitumikia taifa hilo akiwa waziri mkuu mpaka alipoanzisha mfumo wa urais mwaka 1987.

Lakini miaka yake ya kuwa madarakani Zimbabwe imekuwa katika mgogoro mkubwa wa kiuchumi na kutawala kimabavu.Yeyey na wanaomuunga mkono walikuwa madarakani kwa muda mrefu wakitumia vurugu na mauaji kama njama za kushinda chaguzi.

Milioni 231% , kupanda kwa gharama za maisha Julai mwaka 2008

Uchumi wa Zimbabwe umezorota tangu kufanyika mabadiliko ya sera ya ardhi mwaka 2000

Programu hii ilishuhudia wamiliki wa ardhi wazungu wakinyang'anywa ardhi na kupewa raia weusi wa Zimbabwe na wale wenye uhusiano mzuri na wanasiasa, hali hii iliangusha hata uzalishaji nchini humo.

Wakati Benki kuu ya nchini humo ikichapisha pesa kuondoka kwenye mdororo wa kiuchumi, kupanda wa gharama za maisha kukashika hatamu.

Maelezo ya picha,

Chati inayoonyesha kupanda kwa gharama za maisha

Ingawa Benki ya dunia haina takwimu za mwaka 2008 na 2009, Takwimu za benki kuu ya Zimbabwe zinaonyesha gharama za maisha zilipanda na kufikia milioni 231% mwezi Julai mwaka 2008.

Maafisa waliacha kuripoti takwimu za kila mwezi baada ya gharama za maisha kupanda maradufu mwezi Novemba mwaka 2008.

Zimbabwe ililazimika kuachana na matumizi ya sarafu yao mwaka mmoja baadae kwa kiasi cha dola ya zimbabwe quadrillioni 35 kwa dola moja ya Marekani

$16.3bilioni = GDP mwaka 2016

Kipindi cha mwaka 2009 na 2012 kilikabiliwa na changamoto kubwa, imesema Benki ya dunia.Uzalishaji umeshuka kwa wastani wa 8% kutoka mwaka 2009 mpaka 2012, kutokana na biashara kuyumba na ukame.

Rais Mugabe wakati wote amekuwa akilaumu mataifa ya magharibi kuwa matatizo ya kiuchumi ya Zimbabwe yamesababishwa na nchi za magharibi,wakiongozwa na Uingereza ambayo alidai kuwa ilipanga kumuondoa madarakani baada ya kuwanyang'anya wazungu mashamba.

74% ya watu wanaishi kwa chini ya dola 5.50 kwa siku

Hali ya kisiasa na uchumi mbaya nchini humo vimesababisha kuwapo kwa viwango vikubwa vya umasikini.

Miaka migumu kati ya mwaka 2000 na 2008 kulishuhudia viwango vya umasikini kupanda kwa zaidi ya 72%, kwa mujibu wa Benki ya dunia. Moja ya tano ya idadi ya wakazi waliishi kwenye umasikini uliokithiri.

Umasikini uliokithiri, unakadiriwa kushuka tangu mwaka 2009 mpaka mwaka 2014.

Takriban 27% ya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wako katika hali baya ya kiafya kwa sababu ya lishe duni, utafiti wa kiafya nchini humo ulibaini mwaka 2015.

Lakini umasikini nchini Zimbabwe uko chini kuliko nchini ningine zilizo kusini nwa jangwa la Sahara,ambapo 41% ya watu wanaishi kwa kiwango cha chini ya dola 1.90 mwaka 2013.Kwa mujibu wa data za Benki ya dunia.

90% = Kiwango cha ukosefu wa ajira

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Wakulima nchini Zimbabwe

Benki ya dunia ilitoa makadirio yake kwa kutazama data za shirika la kazi duniani iliyoeleza kuwa idadi ya watu wasio na ajira imefikia 90% mwaka huu.

Hata hivyo, Tafsiri ya benki ya dunia imelenga wale ambao wanatafuta kazi.Wengi wao ambao hawajahesabiwa huenda wasiwe wanatafuta kazi ingawa wanataka, wanaona kama nafasi za kazi ni chache au kwa sababu wanakumbwa na vikwazo mbalimbali kama unyanyapaa, masuala ya kitamaduni na kijamii.

89% = kiwango cha elimu kwa watu wazima

Kutokana na uwekezaji mkubwa uliowekwa tangu uhuru,Zimbabwe ina idadi kubwa ya watu wazima wenye elimu barani Afrika, kiasi cha 89%, kwa mujibu wa data za benki ya dunia tangu mwaka 2014.

Ulimwenguni kiwango cha elimu ni asilimia 86 mwaka 2016 na nchi za kusini mwa jangwa la sahara 64%(takwimu za mwaka 2015).

Maelezo ya picha,

Data zinazoonyesha takwimu za kiwango cha elimu Zimbabwe

Karibu wanawake wote na wanaume wenye umri wa miaka 15-49 wana angalau kiwango cha elimu ya msingi, kwa mujibu wa utafiti uliofanyika nchini humo mwaka 2015.Zaidi ya 70% ya watu walio na umri wa miaka 15-49 wamesoma mpaka elimu ya sekondari.

13.5% = Idadi ya watu wazima waishio na virusi vya Ukimwi

Zimbabwe ni nchi ya sita kusini mwa jangwa la sahara ikiwa na idadi ya watu milioni 1.3 waishio na virusi vya ukimwi kwa mwaka 2016, kwa mujibu wa UNAIDS

Hata hivyo, baada ya mwaka 1997, viwango vimekuwa vikishuka.

Maelezo ya picha,

Chati inaonyesha kupanda na kushuka kwa viwango vya watu walio na virusi vya ukimwi nchini Zimbabwe

Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa,haya ni matokeo ya kampeni zilizofanikiwa kuhamasisha matumizi ya mipira ya kiume pia programu za kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.Matibabu na huduma kwa walioathirika zimeboreshwa.

60 =Umri wa kuishi

Umri wa kuishi ulishuka miaka ya 1990, watu walipoteza maisha hasa kutokana na virusi vya Ukimwi.Umri wa kuishi ulishuka kutoka miaka 61.6 mwaka 1986 mpaka 43.1 mwaka 2003

Maelezo ya picha,

Chati inayoonyesha umri wa kuishi Zimbabwe

Kwa sasa hali imetengamaa tena, lakini kutokana na ukosefu wa ajira na umasikini na maambukizi ya Ukimwi, umri wa kuishi umeendelea kuwa miaka 60 mwaka 2015, kwa mujibu wa Data wa Benki ya dunia.

Watu 81 kati ya 100 wanatumia simu za mkononi

Simu za mkononi hutumika sana kama njia ya mawasiliano na raia wa Zimbabwe

Lakini wakati wengi wakiwa na simu za mkononi, 42% ya nyumba zina redio, 37% zina televisheni na 10% zina Kompyuta.Kwa mujibu wa utafiti wa taasisi ya utafiti, Zimbawe Demographic and Health

Maelezo ya picha,

Chati zinaonyesha ongezeko la matumizi ya simu za mkononi nchini Zimbabwe

16.7 million =Idadi ya watu

Baada ya Uhuru mwaka 1980, kupungua kwa idadi ya watoto wanaozaliwa na ongezeko la watu wanaopoteza maisha vimefanya kushuka kwa ongezeko la watu

Kutokana na idadi ya watu wengi wanaoondoka nchini humo, bado idadi ya watu haijafikia ile iliyokuwa baada ya uhuru

Maelezo ya picha,

Chati zikionyesha ongezeko la watu kwa mwaka