Mtu ambaye ana mzio wa mwangaza wa jua

Alex akiwa amevalia kifaa kilichotengezwa na wazazi wake kumlinda dhidi ya jua kali

''Natamani ningeweza kuwa kama mtu mwengine'' .

Hayo ni maneno ya Alex ambaye hajawahi kuona nje tangu alipozaliwa

Kulingana na mamake kijana huyo aliyezaliwa mwezi Machi ,mwanawe ana mzio wa jua .

Mamake anasema kwamba walimpeka Allex nje katika jua baada ya kuzaliwa na dakika 10 baadaye akaanza kutokwa na malengelenge kwenye uso wake wote.

Anasema kuwa walimtoa tena nje na kumuweka katika kivuli siku nyengine na matokeo yake yalikuwa uso wa Allex kutokwa na malengelenge kama ilivyokuwa siku ya kwanza.

''Halikuwa jambo la kawaida kwani licha ya kumtoa tena nje siku nyengine na kumweka katika kivuli matokeo yalikuwa malengelenge uso msima'', alisema mamake.

Allex ana mzio wa jua na iwapo atatoka nje anaweza kuaga dunia. Hivyobasi kwa Allex dunia ilikuwa kama eneo hatari

Mamake aliyetafuta ushauri wa madaktari anasema kuwa waliambiwa watalazimika kulala mchana na kuishi nyakati za usiku ili kukwepa mwangaza wa jua.

Anasema kwamba katika miaka ya kwanza alifunga pazia na madirisha wakati wa mchana na kusalia ndani ya nyumba na mwanaye wakilia huku watu wakiendelea na maisha yao ya kawaida nje.

Wazazi wa Allex waliunda kifaa kinachoweza kumlinda dhidi ya mwangaza wa jua lakini kikawa kinapasuka kwa urahisi na hakikuweza kukidhi mahitaji ya kijana huyo.

Hivyobasi walisikiza ushauri wa mtaalam wa vifaa Zoe Laughlin aliyetaka kubadilisha maisha ya kijana huyo.

Mtaalam huyo aliwatengezea kifaa kinachovaliwa usoni chenye nguvu za kulinda mionzi ya jua, na hatimaye akamsaidia kijana huyo kutoka nje licha ya mwangaza mkali wa jua.

Na alipotoka akiwa amevalia kifaa hicho kwa mara ya kwanza Alex alisema: Sikudhania kwamba ningeweza kutoka nje wakati wa mchana maisha yangu yote.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii