Mtazamo halisi: Ni kwasababu gani baadhi ya nchi za Afrika hazitaki msaada wa nguo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rwanda inapanga kupiga marufuku uagizwaji wa nguo za mitumba kutoka nje

Madai: Kutoa msaada wa nguo za mitumba imekuwa na athari hasi kwa sekta ya viwanda vya nguo katika nchi za Afrika.

Rais wa Rwanda , Paul Kagame, amesema : "Tumewekwa katika hali ambapo ni lazima tuchague - uchague kuwa mwenye kupokea nguo... au uchague kukuza viwanda vyetu vya nguo."

Rwanda inapanga kupiga marufuku uagizwaji wa nguo za mitumba ifikapo mwaka 2019 na tayari imekwishaweka ushuru wa forodha kwa bidhaa hiyo.

Uamuzi uliochukuliwa: Uagizwaji wa nguo kwa bei nafuu kutoka nchi za magharibi kumekuwa na athari kwa watengenezaji wa nguo wa ndani ya nchi - lakini kumekuwa na mabadiliko katika sera za biashara za dunia na kuongezeka kwa watengenezaji wa nguo barani Asia.

Biashara ya nguo pia inawaajiri maelfu ya watu katika baadhi ya nchi.

Nchi za Afrika wakati mmoja zilikuwa na viwanda vikubwa vya utengezaji wa nguo- na baadhi ya wakosoaji wanalaumu kumwagwa Afrika kwa nguo zenye thamani ya chini za mitumba kutoka nchi za magharibi kuwa chanzo cha kuporomoka kwa sekta ya viwanda vya nguo barani.

Biashara ya muda ya mitumba imekuwepo kwa muda mrefu duniani , ikitolewa zaidi kwa maduka ya misaada katika mataifa tajiri ya magharibi h na baadae kuuzwa kwa wafanyabiashara barani Afrika na maeneo mengine dunia.

Hii ni biashara kubwa. Baadhi ya wafanyabiashara wa jumla katika mataifa ya Afrika wameweza kubaini kuwa mitumba ni biashara yenye faida ya juu.

Hata hivyo, baadhi ya nchi za Afrika yamechoshwa na kupewa na madhara yake kwa viwanda vya ndani ya nchi zao.

Mnamo mwaka 2015, nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inayojumuisha nchi za Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda, zilitangaza kwamba zitapiga marufuku uagizwaji wa mitumba kuazia mwaka 2019 ili kulinda viwanda vyao vya nguo.

Nchi za Afrika Mashariki zilichukua 13% ya soko la dunia la nguo za mitumba (lenye thamani ya $274m mnamo 2015), zilianza kuweka ushuru wa forodha.

Rwanda na Marekani katika mgogoro

Lakini wakati huo, kutokana na shinikizo la Marekani, nchi za Afrika Mashariki zilipunguza ushuru nna kusitisha marufuku ya mitumba iliyokuw imependekezwa.

Rwanda, hata hivyo, ilikataa kuondoa marufuku hiyo.

Na mwezi Machi 2018, ikaiondoa Rwanda kwa muda kwenye mpango wake wa kuziwezesha nchi za zilizoko kusini mwa jangwa la sahara kuuza bidhaa zake kwenye soko la Marekani unaofahamika kama AGOA.

Lakini Rwanda haikuyumba na ikashikilia msimamo wake wa kuweka ushuru wa mitumba, ikisema kuwa inataka kujenga sekta yake ya nguo ''zinazotengenezwa Rwanda''

Na matokeo yake, ilipoteza baadhi ya fursa ya kuuza idhaa zake Marekani bila ushuru.

Hata hivyo mpango wa kupiga marufuku uagizwaji wa mitumba haukuungwa mkono na kila mmoja katika nchi hizo, hukusan wale ambao maisha yao yalitegemea sekta ya mitumba.

Mabadiliko ya sera ya biashara duniani

Madai juu ya athari ya biashara ya nguo za mitumba yanapaswa kuangaliwa kwa dhana pana.

Nchi za kiafrika, chini ya shinikizo la Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani (IMF)kwa miaka mingi zimekuwa zikifuata mifumo ya mipango inayoweza kubadilika ambayo imeweza kupunguza kikamilifu ruzuku zilizoandaliwa kwa ajili ya kulinda ukuaji wa viwanda vya ndani na hivyo kuweza kufungua milango yake kwa masoko ya biashara za kigeni.

Hii imewarahisishia wafanyabiashara wa nguo wa Ulaya, Marekani na Asia kuuza bidhaa zao katika bara la Afrika

Kigezo kingene kimekuwa ni kuondolewa kwa masharti ya serikali yanayoweka ukomo wa idadi na thamani ya pesa kwa sekta ya nguo chini ya kile kilichofahamika kama mpango wa Multi-Fibre Arrangement (MFA), ulioanzishwa mnamo mwaka 1975.

Moja ya kanuni za mpango huo ilikuwa ni kuwalinda wazalishaji wa Marekani na Muungano wa Ulaya dhidi ya nguo zenye thamani ya chini zinazouzwa kutoka Asia- lakini makubaliano hayo pia yalikuwa na athari zake katika kuwawezesha wafanyabishara wa Affrika kupata fursa ya kuuza bidhaa zao katika masoko ya Marekani na Uingereza

Image caption Uhaba wa nguo za mitumba kikwazo kwa wanyaruanda

Makubalino haya yaliondolewa taratibu na hatimae kuvunjwa kabisa mwaka 2005.

Hii iliwawezesha watengenezaji wa nguo wa Asia pamoja na wale wa Marekani, Muungano wa Ulaya na Canada, kuingia kwa wingi katika masoko ya Afrika wakiwa na nguo zote mpya na za kuukuu

Ilipofika kwaka 2005, Shirikisho la Kimataifa la Wafanyakazi Viwanda vya nguo, Nguo na Ngozi lilikadiria kwamba zaidi ya ajira 250,000 katika sekta hiyo zimepotea barani Afrika.

Kuanguka kwa sekta ya nguo

Hakuna takwimu za hivi karibuni za sekta ya nguo duniani

Hata hivyo, utafiti wa Ujerumani wa mwaka 2006 ulioangazia sekta hii kusini mwa jangwa la sahara uliripoti kuwa uzalishaji wa Ghana ulipungua kwa karibu 50% baina ya 1975 na 2000.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bidhaa nafuu zinazoagizwa kutoka Asia pia zimekuwa na athari

Nchini Zambia, kiwango cha ajira katika sekta ya viwanda vya nguo kilishuka kutoka 25,000 miaka ya 1980s hadi ajira 10,000 mwaka 2002, ilisema.

Kuna sababu nyingine kando na mabadiliko ya kibiashara na biashara ya nguo za mitumba.

Mzozo na utulivu wa kisiasa[ia vimechangia katika baadhi ya maeneo.

Kwa mfano, katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, kutokana na vita vya miaka vya wenyewe kwa wenyewe , kulikuwa na upungufu wa zaidi ya 80% wa uzalishaji wa nguo kati ya mwaka 1990 na 1996.

Ni zipi athari za kuweka ushuru wa mitumba?

Tangu Rwanda iweke ushuru wa nguo za mitumba zinazoagizwa kutoka nje, takwimu za serikali zinaonesha kuongezeka kwa thamani ya nguo zinazotengenezwa na viwanda vya ndani ya nchi imeongezeka kwa kiwango cha kati ya $7m na $9m.

Vi vigumu kuonyesha uhusiano wa moja kwa moja kati ya viwango vipya vya ushuru na ongezeko, kwasababu pia kumekuwa na uwekezaji kutoka nje ya nchi kwenye sekta hiyo.

Watengenezaji wa nguo wa Kichina C&H Garments walifungua kiwanda chao nchini rwanda mnamo mwaka 2015.

Na kwa sasa kinawaajiri Wanyarwanda wapatao 1,400 , ambao huzalisha nguo kama sare za polisi na jeshi.

Lakini sekta ya viwanda vya nguo nchini Rwanda ni ndogo kiuchumi.

Ni muhimu kusema kuwa sekta ya nguo za mitumba ni muajili mkubwa katika Afrika Mashariki, wa moja kwa moja ama kwa njia isiyo ya moja kwa moja hasa katika mauzo na usambazaji wa bidhaa hiyo.

Kwa hivyo basi, wakati uagizwaji wa nguo za mitumba kutoka nje unapunguza uzalishaji na biashara ya ndani, ni dhahiri kuwa pia hutoa ajira- na wazalishaji wa ndani wa nguo wanapinga nguo nafuu na zinazopatikana kwa urahisi za Asia na maeneo mengine.

Mwishi, ni muhimu kutambua kuwa lichaya biashara ya dunia ya mitumba ambayo bado ni biashara kubwa, inaonyesha dalili ya kukataliwa kama sehemu ya biashara na kuna mabadiliko ya tabia za ununuzi

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii