Kwa nini mwezi unabadilika rangi baada ya kupatwa?

Tukio la kupatwa kwa mwezi la tarehe 27 Julai 2018 litakuwa la muda mrefu zaidi karne ya 21

Kupatwa kwa mwezi kutaanza polepole mwendo wa saa mbili na robo saa za Afrika mashariki na inatarajiwa kwamba raia wa Tanzania na wenzao wa Kenya wataweza kuliona tukio hilo la kihistoria ambalo litakuwa la muda mrefu zaidi katika karne ya 21.

Mwezi utaanza kupatwa muda huo huku ukipatwa kamili mwendo wa saa nne na nusu ambapo utabadilika na kuwa mwekundu.

Kutoka saa nne na nusu Tukio hilo litaendelea kwa dakika 51 na moja ambapo kukamilika kwa tukio hilo la kihistoria kutaanza na baadaye kuendelea hadi saa sita na dakika 13 ambapo litakwisha.i

Tukio hilo litakuwa la muda mrefu zaidi katika karne ya 21, kulingana na shirika la usimamizi wa anga za juu(NASA).

Na iwapo una bahati utafanikiwa kuona tukio hilo kwa saa moja na dakika 43.

Je kupatwa kwa mwezi ni nini?

Kupatwa kwa mwezi hutokea wakati jua, dunia na mwezi zinapokua kwenye mstari mmoja.

Hii inamaanisha kwamba dunia iko katikati ya jua na mwezi hatua inayoziba mwanga wa jua.

Kupatwa huko hutokea wakati mwezi unapoingia katika kivuli cha dunia.

Katika awamu tofauti kupatwa huko kwa mwezi kutafanyika kwa saa tatu na dakika 55.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Usiku wa kupatwa kwa mwezi hushirikishwa na uzushi wa kuwepo kwa 'mwezi wa damu' kutokana na rangi yake nyekundu.

Kwa nini unaitwa 'mwezi wa damu'?

Usiku wa kupatwa kwa mwezi hushirikishwa na dhana na wa kuwepo kwa 'mwezi wa damu' kutokana na rangi yake nyekundu.

Hilo linatokana na athari za kutazama miale ya jua katika anga na rangi za machungwa na nyekundu zinazoonekana katika mwezi.

Wakati huohuo , wakati wa kupatwa kwa mwezi mnamo tarehe 27 Julai, mwezi utakuwa mbali na zaidi kutoka kwa dunia.

Ni lini na wapi utaonekana?

Kupatwa kwa mwezi mnamo tarehe 27 Julai kutaonekana Ulaya, Afrika, mashariki ya kati , katikati mwa Asia na Australia ikiwa ni maeneo yote isipokuwa kaskazini mwa Marekani.

Hautalazimika kutumia darubini kuutazama mwezi huo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kivuli cha tukio hilo kitaonekana katika setlait bila kuziba mwangaza wote. Nchini Uingereza hautaweza kuona mwanzo wa tukio hilo

Nani atakayeuona vizuri zaidi?

Eneo zuri la kulitazama tukio hilo ni eneo nusu ya Mashariki mwa Afrika ,Mashariki ya kati na katikati mwa bara Asia.

Tukio hilo halitaonekana katika maeneo ya kati na Marekani Kaskazini.

Kusini mwa Marekani , unaweza kuonekana kiasi katika maeneo ya mashariki hususan miji ya Buenos Aires, Montevideo, Sao Paulo na Rio de Janeiro.

Katika miji mingine ya karibu utaonekana wakati mwezi utakapokuwa ukiondoka katika eneo hilo-huo ni mstari ambao ardhi na anga zinaonekana kukutana.

Kivuli cha tukio hilo kitaonekana katika satelaiti bila kuziba mwangaza wote.

Nchini Uingereza hautaweza kuona mwanzo wa tukio hilo, hiyo ni kwa sababu mwezi utakuwa chini ya upeo wa macho.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii