Cecilia Wangari : Ajuza wa miaka 82 ambaye ni fundi stadi wa redio za magari Kenya

Cecilia Wangari : Ajuza wa miaka 82 ambaye ni fundi stadi wa redio za magari Kenya

Cecilia Wangari au (Shosh) kama vile wengi wanavyomfahamu ni bibi wa miaka 82 ambaye amepata umaarufu kwa haraka hasa mjini Nairobi nchini Kenya.

Kinyume na bibi wengine walio na umri sawa na wake ambao mara nyingi huishi vijijini wakiwategemea watoto wao au hata wajukuu kuwalisha, kwake Cecilia ni tofauti kabisa.

Cecilia ni fundi wa radio za magari! ndio fundi wa redio za magari.