Ubalozi wa Marekani mjini London unapiga mnada karatasi za usafi chooni na vifaa vingine chakavu

Picha ya mashine ya kufuta vumbi na pakiti ya karatasi za usafi wa chooni

Chanzo cha picha, US State Department

Maelezo ya picha,

Moja ya mashine za kufuta vumbi kadhaa zilizovunjika na pakiti za karatasi za usafu wa msalani vinavyouzwa na kwenye mnada wa balozi wa Marekani

Ubalozi wa Marekani mjini London uhnapiga mnada vifaa visivyo hitajika kwasababu unatarajia kuhamia kwenye makazi mapya yenye thamani ya $1bn (£762m) yaliyoko eneo la Vauxhall.

Miongoni mwa bidhaa zinazouzwa ni: mashine za kufuta vumbi ambazo zinahitaji kukarabatiwa, gari lililotumiwa na karatasi 1,200 za usafi wa chooni.

Hakuna kifaa hata kimoja kilicho na nembo rasmi ya Marekani au thamani yake ya kihistoria.

Ubalozi wa Marekani ulihamisha ofisi zake kutoka eneo la Mayfair mwezi wa Januari, lakini mchakato wa kuhama ulianza mwaka 2008 chini ya utawala wa George W Bush kwa sababu za hofu ya kiusalama.

Wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani hivi karibuni ilituma orodha ya makumi kadhaa ya vifaa vyake visivyotakikana kwenye mtandao kwa ajili ya kupigwa mnada , na wanunuzi wana hadi tarehe 8 Agosti kuwasilisha maombi yao ya kuvinunua.

Karatasi za usafi wa chooni (toilet paper rolls) - ambazo zinazouzwa zimewekewa bei ya $199.

Gazeti la The Independent limeitaja bei iliyowekwa kwa mnada wa karatasi za usafi wa chooni kuwa "inayoweza kuwa ya juu kidogo kuliko kiwango cha kawaida".

Kwa wale wanaotaka kununua bidhaa hizo zisizotakikana za ubalozi wa Marekani , kuna gari aina ya Volvo 2007 "iliyotumika " inayouzwa $8,427.

Pia kuna mashine tano za kufuta vumbi zilizovunjika aina ya Dyson ambazo zinauzwa kwa thamani ya $1 na $65, ama taa mpya za mezani aina ya LED kwa bei ya $75.

Ubalozi ulihama kutoka eneo la Mayfair kwasababu ulikuwa mdogo kiasi cha kutoweza kukidhi mahitaji ya kisasa ya kiusalama yalinayohitajika.

Jengo jipya la ubalozi lilifunguliwa Januari 16.

Mwezi wa Januari Rais Donald Trump aliahirisha ziara yake kwenye ubalozi mpya , akiyataja kuwa mkataba mbaya wa makazi.

Marekani iliuza jengo la zamani la ubalozi wake kwa kampuni ya ujenzi wa makazi ya Qatari real estate group Qatari Diar, ambayo inatarajia kulibadili jengo hilo kuwa hotel.

Jengo la zamani halikuwa mali ya Marekani moja kwa moja .

Ilikuwa na kibali cha kulimilikicha miaka 999 , lakini mmiliki mkuu ni kampuni ya Grosvenor Estates.

Uamuzi wa kuhama kwa ubalozi huo ulichukuliwa na utawala wa George W Bush mwezi Oktoba 2008, muda mfupi kabla ya kuondoka madarakani.

Gharama ya mwisho ya jengo la ubalozi wa zamani haikufichuliwa, lakini awali jengo hilo lilikisiwa kuwa na thamani ya disckati ya £300m na £500m.