Moise Katumbi: Msafara wa kiongozi wa upinzani wazuiwa kuingia DR Congo

Moise Katumbi aliondoka DRC mnamo Mei 2016, siku moja baada ya kutolewa waranti ya kukamatwa kwake Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Moise Katumbi aliondoka DRC mnamo Mei 2016, siku moja baada ya kutolewa waranti ya kukamatwa kwake

Msafara wa kiongozi wa upinzani nchini DR Congo Moise Katumbi umerudi nchini Zambia baada ya serikali ya DR Congo kumzuia kuingia nchini humo.

Alikuwa amekwama mpakani kati ya mataifa hayo mawili kwa saa kadhaa .

Mwandani huyo wa karibu wa rais Kabila amekuwa akiishi mafichoni kwa miaka miwili na alikuwa na matumaini ya kurudi nyumbani ili kuwania urais.

Awali kiongozi huyo alikuwa amevuka na kuingia eneo lisilodhibitiwa na nchi yoyote kati ya mpaka wa zambia na taifa la DR Congo huku maelfu ya wafuasi wake wakielekea katika eneo hilo kumlaki.

Alikuwa katika mji wa Kasumbalesa, kulingana na mwandishi wa BBC Anne Soy. Awali tuliwanukuu wafuasi wake wakisema kuwa alikuwa amevuka mpaka na kuingi nchini DR Congo.

Mji wa Kasumbalesa upo takriban kilomita 95 karibu na nyumbani kwao Lubumbashi.

Vikosi vya DR Congo vilifyatua risasi hewani kuwatawanya wafuasi wake waliosubiri kumkaribisha akijaribu kuvuka mpaja kulingana na mwandishi wa BBC Poly Muzalia.

Wafuasi wake wanasema alikuwa amevuka mpaka na kuingia nchini humo akiabiri gari lililotoka Zambia licha ya utawala wa taifa hilo kutishia kumkamata iwapo angejaribu kurudi nyumbani.

Kundi la chama cha bwana Katumbi Ensemble pour le Changement, lilichapisha kanda ya video ya bwana katumbi akiwa katika eneo la Kasumbalesa , mji wa mpakani nchini DR Congo.

Moise Katumbi, alikuwa amezuiwa kurudi nchini kugombea urais katika uchaguzi mkuu Desemba mwaka huu.

Serikali ya Congo imemzuia Gavana huyo zamani wa jimbo la Katanga anayeishi uhamishoni Afrika kusini kurudi nyumbani.

Katumbi aliomba ruhusa kuingia nchini leo asubuhi kuwahi kuwasilisha makaratasi yake ya uteuzi wa chama kuwa mgombea urais kwa tume ya uchaguzi nchini.

Sababu za Moise Katumbi kuanzisha Chama akiwa Afrika Kusinihttps://www.bbc.com/swahili/medianuai/2016/03/160308_katumbi

Maafisa wa polisi huko Lubumbashi wameweka vizuizi katika bara bara kuu na usalama umeimarishwa ndani na katika maeneo yalio karibu na uwanja wa ndege.

Kuna mipango ya kuzifunga njia za ndege kutua kuizuia ndege ya Katumbi isitue DRC.

Image caption Bw Katumbi pia ni Rais wa klabu ya soka maarufu katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ya TP Mazembe.

Moise Katumbi ni nani?

 • Jina lake la mwisho pia Tshapwe
 • Anajulikana kama Moses Katumbi nchini Zambia, ambapo aliishi kwa miaka mingi
 • Tarehe ya kuzaliwa 28 Disemba 1964
 • Eneo la kuzaliwa ni Kashobwe
 • Ni kabila la Babemba
 • Ni kaka wa kambo wa Katebe Katoto, maarufu kama Rafael Soriano, na mfuasi wa Laurent Nkunda
 • Baba yake ni Padre Nissim Soriano, Mitaliano Myahudi kutoka Rhodes
 • Mama yake ni Virginie Katumbi, kutoka familia ya kifalme ya Kazembe
 • Rais wa kalbu ya Soka TP Mazembe Football iliopo Lubumbashi
 • Anajullikana kwa mapenzi yake na kofia za mtindo 'Cowboy'

Waziri wa habari Lambert Mende anasema gavana huyo wa zamani kutoka jimbo lenye utajiri mkubwa wa madini atakamatwa iwapo atajaribu kuingia nchini kwa ndege ya usafiri wa abiria.

Katumbi aliondoka nchini Congo mnamo 2016 baada ya kukosana na rais Joseph Kabila.

Baadaye alishtakiwa kwa udanganyifu wa mali na alihukumiwa miaka mitatu gerezani pasi yeye kuwepo mahakamani.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Makamu wa rais wa zamani DRC Jean -Pierre Bemba akiwasili Kinshasa

Kiongozi mwingine wa upinzani - Jean-Pierre Bemba - alirudi DRC siku ya Jumatano baada ya kutokuwepo kwa zaidi ya muongo mmoja.

Aliwasilisha makaratasi yake ya kugombea urais hapo jana Alhamisi.

" Ninaweza kuthibitisha kuwa nilikuwa na kadi ya kupiga kura, na nimewasilisha nyaraka zote," shirika la habari AFP linamnukuu Bemba akizungumza nje ya makao makuu ya tume ya uchaguzi.

Kurejea kwa Bemba DRC kutakuwa na maana gani?

Hatahivyo chama tawala kimesema hafai kugombea kutoana na kushtakiwa kwa rushwa katika mahakama ya kimataifa ya jinai ICC. Amekataa rufaa kupinga kesi hiyo.

Haki miliki ya picha Getty Images

Jean-Pierre Bemba ni nani?

 • Mfanyabiashara mwenye ushawishi mkubwa na mwanawe mfanyabiashara maarufu Congo Bemba Saolona
 • 1998: Alisaidiwana Uganda kuunda MLC - kundi la waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
 • 2003: Ateuliwa makamu wa rais chini ya mkataba wa amani
 • 2006: Ashindwa na rais Joseph Kabila katika duru ya pili ya uchaguzi lakini apata kura nyingi magharibi mwa Congo ukiwemo mji wa Kinshasa
 • 2007: Atoroka kwenda Ubelgiji baada ya mapigano kuzuka Kinshasa
 • 2008: Akamatwa Brussels na kuwasilishwa ICC
 • 2010: Kesi inaanza
 • 2016: Apatikana na hatia kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadamu
 • 2018: Hukumu inabadilishwa baada ya kukatwa rufaa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii