Babu kutoka India anayeliombea tango refu zaidi duniani lizidi kukua Uingereza

Raghbir Singh Sanghera giant cucumber
Image caption Raghbir Singh Sanghera

Babu mmoja huko Derby, Uingereza, anasema kuliombea tango lake imechangia liwe refu hadi kufikia kuvunja rekodi ya dunia.

Raghbir Singh Sanghera, ambaye alikuwa mkulima nchini India kabla ya kuhamia Uingereza mwaka 1991 anasena tango lake limekua hadi urefu wa sentimita 129.54.

Bw Sangher alisema tango lake ambalo familia yake haujikani bado linazidi kukua kwa urefu na unene.

Rekodi ya sasa ya Guinness ya tango refu zaidi duniani ambalo lilikuwa huko Wales mwaka 2011 ilifikia urefu wa sentimita 107.

Peter Glazebrook, mtaalamu wa masuala ya kukuza mboga kubwa anasema tango hilo linaonekana kuwa la familia ya (Cucumis meloflexuosus), la kutoka Marekani na si lile la (Cucumis sativus).

Image caption Tango hili sasa limefikia urefu wa sentimita 129.54

Bw Sanghera anasema atalipeleka tango hilo huko Singh Sabha Gurdwara, Nottingham, kwa kila mtu kula wakati litakuwa tayari kuliwa.

"Bado linakua na litanenepa, kisha litakapokuwa tayari tutaweka tembe kwa mwaka ujao," babu huyo wa miaka 75 alisema.

"Ni lazima ulitunze kama mtoto."

Image caption Bw Sanghera an sehemu ya kuketi karibu akiomba

Bw Sanghera anasema mboga hiyo ilikuwa kati ya nne alipanda miezi minne iliyopita, lakini baada ya zingine tatu kuliwa hilo likabaki kukua.

"Nimetengasehemu ya kuketi karibu nalo ambapo ninaliona na kulitazama," alisema.

"Ninaomba kuwa litakuwa, kuwa litatuweka na afya nzuri na kuwa kila mmoja awe na afya na furaha, linaniletea raha nikilitazama.

Mada zinazohusiana