Nidhamu ya matumizi ya simu: Mambo matano ya kukuepusha kuwakera wengine

Mashabiki wakitumia simu zao wakati wa tamasha Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mashabiki wakitumia simu zao wakati wa tamasha

Ni kitu cha kwanza wengi wetu tunakitazama asubuhi na kitu cha mwisho kukiangalia usiku.Simu zetu haziko mbali nasi na tunaziangalia kila baada ya dakika 12, kwa mujibu wa mamlaka ya kudhibiti mawasiliano nchini Uingereza, Ofcom.

Ni mahusiano ambayo yanaonekana kuwa yatadumu zaidi, hivyo tunakudokeza sheria tano za matumizi ya simu ambayo yanapaswa kutazamwa kwa umakini.

1.Kuzungumza na simu wakati wa kula chakula

Watu wengi hufanya hivyo, na zaidi ya 26% ya vijana wanakubali suala hili

''Simu zinapaswa kuwa zimezimwa saa zote wakati wa chakula, mikutano na sherehe,''anasisitiza Diana Mather, mshauri wa masuala ya tabia.

''Mtu uliyenaye ni mtu aliye muhimu zaidi.Hakuna miongoni mwetu asiye na umuhimu.

Hata kutazama televisheni inakuwa imezimwa kwa baadhi ya watu wakati mkiwa kwenye meza ya chakula

Zaidi ya watu wanne kati ya watano walio na umri wa miaka 55 na zaidi wanafikiri haikubaliki kutazama ujumbe wa simu ukilinganisha na 46% ya umri wa miaka 18 mpaka 34.

2. Kusikiliza muziki wenye sauti kubwa kwenye usafiri wa Umma

Kitaalamu huitwa sodcasting yaani tabia ya kusikiliza muziki kutoka kwenye simu au vifaa vingine kwa sauti kubwa bila kujali wanaokuzunguka.

Inahusisha kutazama video au kucheza michezo ya kwenye simu kwa sauti kubwa.

76% kati yetu tunalipinga lakini hatuachi tabia hiyo.

3.Kuzungumza na simu wakati unapotakiwa kumsikiliza mtu mwingine

''Kutuma ujumbe na kuzungumza ni tabia mbaya sana,''anasema mtaalamu Diana Mather.

Ikiwa hatupeani muda sisi wenyewe, tunapoteza nafasi kubwa sana ya kufahamiana vizuri''.

Wanasiasa wenzake John McDonnell huenda walikosa kumfahamu kansela kivuli wakati wa kipindi cha bunge la commons kikiendelea

Alikuwa na cha kusema wakati wa kutoa taarifa mwaka 2016 lakini wenzake walikuwa wakitazama simu zao za mkononi.

Image caption Wabunge wakitazama simu zao

4. Kutembea huku ukitazama simu yako

Huinamisha vichwa, macho yakiwa kwenye kioo cha simu, wanakuja upande ambao upo.Kimoyomoyo unapiga kelele tazama mbele! tazama mbele!

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanamke akiwa makini kwenye simu yake

Na mtumiaji wa Twitter @tiredhorizon ametoa onyo kwa Umma weka simu yako mbali unapokuwa kwenye majengo ya umma, hospitali na karibu na maeneo magari aina ya malori yanapogeuza.

Alisema amekuwa akishuhudia watu wakijigonga kwenye mbao za matangazo, au wakiwagonga wagonjwa wakiwa kwenye vitanda hospitalini.

5. Kutazama simu yako wakati ukiwa na wengine mkitazama televisheni

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Familia ikitazama televisheni wakati wakiwa na vifaa vya mawasiliano

Kati ya watu 10, wanne (41%) ya watu wazima wanaona kuwa haikubaliki kutumia simu wakati uko na familia kwenye sofa mkitazama televisheni.