Mwanafunzi wa chuo aliyepigwa picha za kufuzu akiwa na mamba Marekani

Makenzie leans into alligator

Chanzo cha picha, Makenzie Noland

Maelezo ya picha,

Mwanafunzi huyu amekuwa akipata mafunzo kwenye kituo cha kuwatunza wanyama cha Beaumont

Mwanafunzi wa chuo kimoja nchini Marekani alihakikisha kuwa picha za sherehe yake ya kufuzu zitakuwa za kukumbukwa baada ya kupigwa picha na mamba wa urefu wa mita nne.

Makenzie Noland ni mwanafunzi kwenye chuo cha Texas A&M ambaye atafuzu mwezi Aprili na shahada katika masuala ya sayansi ya wanyama wa porini na viumbe wa majini.

Mwanafunzi huyo amekuwa akipata mafunzo kwenye kituo cha kuwatunza wanyama cha Beaumont ambapo ni makoa wa mamba 450 na wanyama wengine.

Lakini Makenzie na mamba mmoja kwa jina Tex wamekuwa na uhusiano maalumu tangu ajiunge na kituo hicho mwezi Mei.

Anasema anaitikia jina lake na ishara za mikono yake anaapoingia kwenye kidimbwi kumlisha.

Chanzo cha picha, Makenzie Noland

Maelezo ya picha,

Mamba Tex

"Ninaingia kwenye kidimbwi naye kila siku, ni rafiki yangu mkubwa, aliiambia BBC.

Mwanafunzi huyo mwenye miak 21 alikulia huko Bellevue, Nebrasa ambapo kumuona mamba ni ndoto lakini kwa sasa anawahudumia mamba kila siku.

"Tangu nikiwa mdogo nilikuw nashika nyoka na wanyama wengine, nikizungumza na watoto na kuelimisha umma, anaeleza kuhusu mapenzi yake kwa wanyama wa porini.

Alitarajia picha hizo zingeonyesha kile ambacho amekuwa akifanya msimu wa joto.

Chanzo cha picha, Makenzie Noland

Maelezo ya picha,

Anatarajia kuendelea kufanya kazi na sekta ya wanyamapori baada ya kufuzu.

Makenzie anasema amefurahishwa na maoni ya watu kutokana na picha zake ambazo zimesambazwa mara nyingi.

"Sikutarajia hili, lengo langu lilikuwa ni kuchapisha picha nzuri kwenye Instagram."

Anatarajia kuendelea kufanya kazi na sekta ya wanyamapori baada ya kufuzu.