Jinsi kandanda inavyotumika kukabiliana na ndoa za mapema na Ukeketaji
Huwezi kusikiliza tena

Jinsi kandanda inavyotumika kukabiliana na ndoa za mapema na Ukeketaji

'Ingekuwa chaguo la rahisi kusalia mjini Nairobi, kuwa wakili na kupata mapato mazuri, mbali na kuendesha gari zuri aina ya Mercedes benz.lakini nataka kurudi nyumbani''.Ni maisha ambayo fatuma Abdulkadir Adan angeishi. Lakini badala yake akachagua kandanda katika eneo ambapo ni makosa kwa wasichana kucheza soka. ''Nilipigwa mawe na mateke ili nitoke katika uwanja'', alisema katika juhudi zake za kwanza miaka 10 iliopita wakati alipoanzisha timu ya wasichana katika kaunti ya kaskazini mwa kenya ya marsabit. Muda tu baada ya kurudi kutoka katika mchuano huo, wasichana wanane kati ya 12 katika timu yake walitekwa nyara na kulazimishwa kuingia katika ndoa. Ulikuwa mwanzo mbaya. Fatuma alianzisha shirika lisilokuwa la kiserikali la the Horn of Africa Development Initiative ama HODI kwa jina maarufu, mwaka 2003. Alitaka kutumia soka kuwaleta watu pamoja na kubadilisha tamaduni potovu. Alitumia kandanda kuwavutia vijana wadogo wa kiume baada ya mauaji ya kinyama ya mwaka 2005 kati ya makabila kadhaa yaliosababaisha mauaji ya watu 100. Ilikuwa bunduki aina ya AK-47 iliotumika sana badala ya timu ya soka. Na muda mfupi, vijana wadogo hawakuachana na silaha pekee bali pia walikuwa wameanza kucheza dhidi ya wavulana kutoka katika makabila waliotarajiwa kuyachukia.

Mada zinazohusiana