Fatuma Abdulkadir Adan: Mwanamke anayekabiliana na ndoa za mapema kupitia kandanda Kenya

Fatuma Abdulkadir Adan anatumia soka kukabiliana na utamaduni kama vile ukeketaji Haki miliki ya picha FATUMA ABDULKADIR ADAN

''Ingekuwa chaguo la rahisi kusalia mjini Nairobi, kuwa wakili na kupata mapato mazuri, mbali na kuendesha gari zuri aina ya Mercedes benz.

Lakini nataka kurudi nyumbani''.Ni maisha ambayo fatuma Abdulkadir Adan angeishi.lakini badala yake akachagua kandanda katika eneo ambalo ambapo ni makossa kwa wasichana kucheza soka.

Nilipigwa mawe na mateke ili nitoke katika uwanja, alisema katika juhudi zake za kwanza miaka 10 iliopita wakati alipoanzisha timu ya wasichana katika kaunti ya kaskazini mwa kenya ya marsabit.

Haki miliki ya picha FATUMA ABDULKADIR ADAN

Muda tu baada ya kurudi kutoka katika mchuano huo, wasichana wanane kati ya 12 katika timu yake walitekwa nyara na kulazimishwa kuingia katika ndoa.

Ulikuwa mwanzo mbaya.Fatuma alianzisha shirika lisilokuwa la kiserikali la the Horn of Africa Development Initiative ama HODI kwa jina maarufu, mwaka 2003.

Alitaka kutumia soka kuwaleta watu pamoja na kubadilisha tamaduni potovu. Alitumia kandanda kuwavutia vijana wadogo wa kiume baada ya mauaji ya kinyama ya mwaka 2005 kati ya makabila kadhaa yaliosababaisha mauaji ya watu 100.

Ilikuwa bunduki aina ya AK-47 iliotumika sana badala ya timu ya soka.Na muda mfupi,vijana wadogo hawakuachana na silaha pekee bali pia walikuwa wameanza kucheza dhidi wavulana kutoka katika makabila waliotarajiwa kuyachukia.

Wakati fatuma alipoanza kuzungumza na wasichana hao lengo lake lilikuwa kukamiliana na matatizo maalum ikiwemo ndoa za mapema pamoja na ukeketaji.

Mpango wake , kwa jina kuvunja kimya , umewafanya wasichana 1645 kutoka vijiji 152 katika eneo la Marsabit nchini Kenya kucheza soka kwa muongo mmoja.

Kuwawezesha watoto hao kujisimamia kumekuwa jukumu lake kubwa , hususan katika eneo ambapo familia ya kitamaduni na ukabila unawafanya watoto na wanawake kuona kana kwamba hawana sauti.

Mbeleni ilikuwa sawa kwa mtoto wa miaka 13 au 12 kuolewa , fatuma anelezea . leo iwapo utamuoza mtoto wa miaka 13 wasichana katika darasa lake watalalamika mbali na wavulana pia.

Huku FGM na ndoa za mapema zikiwa haramu nchini Kenya , tamaduni zilizopo zina nguvu na mila na desturi zipo.fatuma amelazimika kufanya bidii ili kuhoji tamaduni hizo na vilevile kufanya kazi nazo. Mpango wake umeanza kuzaa matunda.

Baada ya kujadiliana na viongozi wa dini vile atakavyoweza kuunda jezi za wasichana Waislamu wanaotaka kucheza, Hodi sasa inaendesha timu ya wasichana katika Madrassa. 'Siamini kwamba niko hai kuona hilo likifanyika'.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii