Shambulizi la Skripal: Marekani kuiwekea vikwazo Urusi, kuanzia Agosti

Sehemu ya mji wa Salisbury ilizingirwa kuzuia kusambaa kwa kemikali hiyo
Image caption Sehemu ya mji wa Salisbury ilizingirwa kuzuia kusambaa kwa kemikali hiyo

Marekani imepanga kuweka vikwazo vipya kwa Urusi ikiwa ni kujibu kitendo cha shambulizi la sumu la afisa wa zamani wa usalama wa Urusi Sergei Skripal na mtoto wake wa kike nchini Uingereza.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Heather Nauert, amesema nchi yake imegundua kuwa Urusi ilitumia kemikali hatari kumshambulia Skripal na binti yake wa kike jambo ambalo ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa.

Hii ni mara ya tatu Marekani inaiwekea vikwazo nchi fulani kwa kukiuka sheria hii.

Image caption Polisi iliweka vizuizi sehemu zote

Serikali ya Uingereza imeunga mkono suala hilo.

Urusi mara kwa mara imekua ikikanusha tuhuma hizi.

Vikwazo hivi vinatarajiwa kuaza mwishoni mwa mwezi Agosti.

Image caption Skripal na binti yake Yulia walikutwa wamepoteza fahamu baada ya shambulizi hilo

Katika taarifa iliyotolewa Jumatano , wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilithibitisha kuchukua hatua dhidi ya Urusi kuhusiana na tukio la uvamizi kwa kutumia sumu ya kemikali kwa Sergei Skripa na binti yake lililofanyika nchini Uingereza.

Msemaji wa wizara hiyo Heather Nauert amesema imegundulika kuwa Urusi ilitumia sumu hiyo kinyume cha sheria za kimataifa.

Serikali ya Uingereza imeopongeza hatua hiyo kwa kusema ilistahili kwa nchi ambayo inatabia zisizo za kiungwana na ambazo hazivumuliki.

Image caption Wanausalama wa Uingereza wakijizuia na sumu hiyo

Vikwazo hivyo vipya vinatarajia kuanza Agosti 22 vikigusia zaidi uzuiaji wa vifaa vya umeme na teknolojia nyingine kwenda na kutoka Urusi.

Marekani inasema vikwazo vingine vingi zaii vinatarajia kufuata iwapo Urusi itashindwa kuuthibitishia ulimwengu kuwa itaacha mara moja matumizi ya kemikali za aina hiyo.

Hii ni mara ya tatu Marekani kuweka vikwazo kwa nchi iliyotumia kemikali katika mashambulizi dhidi ya binaadam, ikifanya hivyo kwa Syria na Korea Kaskazini.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii