Aurelia Brouwers: Mwanadada anayesaidiwa kujitoa uhai na madaktari nchini Uholanzi

Haki miliki ya picha Ronald Hissink
Image caption Aurelia Brouwers

Mwezi Januari mwanamke mmoja wa Uholanzi alikunywa sumu aliyopewa na Daktari kisha akalala akisubiri kifo chake.kukatishwa uhai kwake kilikuwa kifo ambacho kiliidhinishwa na serikali.Lakini Aurelia Brouwers hakuwa katika hali mbaya ya ugonjwa-aliruhusiwa kukatisha maisha yake kutokana na maradhi ya akili.

''Nina miaka 29 na nimechagua kujitolea kutolewa uhai.Nimechagua kifo kwa sababu nina matatizo ya afya ya akili.Ninateseka sana bila matumaini .Kila pumzi nayovuta ni mateso...''

Kikosi cha Televisheni nchini Uholanzi , RTL kilikaa kwa majuma mawili kikimrekodi Aurelia akiwa anakaribia siku zake za kuondoka duniani-saa nane mchana siku ya Ijumaa, tarehe 26 mwezi Januari.Kwenye ubao mweupe nyumbani kwake alizungushia alama kwa wino mzito mweusi siku zilipokuwa zikisogea kuelekea kifo chake.

Katika kipindi cha majuma ya mwisho, alitumia muda wake na wapendwa wake, pia alitembelea eneo ambalo alilichagua kufanyika shughuli za mazishi.

Huwezi kusikiliza tena
Aurelia Brouwers alitembelea eneo atakapofanyiwa mazishi

Kukatisha uhai kutokana na maumivu au maradhi yasiyotibika ni kinyume cha sheria katika nchi nyingi, lakini nchini Uholanzi inaruhusiwa kama daktari atajiridhisha kuwa mgonjwa anateseka sana kukiwa hakuna matarajio ya kupata nafuu na kama hakuna njia mbadala kwa ajili ya kumpatia nafuu mgonjwa.

Watu 6,585 walikatishwa uhai Uholanzi mwaka 2017 miongoni mwao 83 kutokana na maradhi ya akili.

Aurelia Brouwers alitamani kufa kutokana na historia ndefu ya maradhi yake.

"Nilipokuwa na miaka 12 nilipata msongo wa mawazo .Na nilipofanyiwa uchunguzi ni liambiwa kuwa nina maradhi ya akili, nilikuwa sina furaha, mwenye mawazo ya kujikatisha uhai, msongo wa mawazo, mtu nisiye na furaha na mwenye kusikia sauti mithili mtu ninayesemeshwa''.

Madaktari wa Aurelia hawakuidhinisha maombi yake ya kutaka kukatishwa uhai.Hivyo alipeka ombi lake kwenye hospitali nyingine mjini The Hague iitwayo Levenseindekliniek yaani ''mwisho wa maisha''.Mahali hapo ni matumaini ya mwisho kwa wale ambao maombi yao yalikataliwa na madaktari wao.Hospitali hiyo ilikubali kuidhinisha vifo vya watu 65 kati ya 83 wenye matatizo ya akili mwaka jana, ingawa 10% pekee huwa inaidhinishwa na mchakato huu unaweza kuchukua miaka kadhaa.

''Wagonjwa wenye matatizo ya akili ni watu wenye umri mdogo, ''anasema daktari Kit Vanmechelen,daktari anayewatathimini waombaji na kukatisha uhai wao, lakini hakuhusika kwenye kifo cha Aurelia.

''Aurelia ni mfano wa mwanamke mwenye umri mdogo.Hivyo inakuwa vigumu kufanya uamuzi wa kukatisha uhai kwa kuwa maisha na ndoto nyingi za mtu zinapotea.

Haki miliki ya picha RTL Nieuws, Sander Paulus
Image caption Aurelia Brouwers

Katika kipindi cha majuma mawili ya mwisho ya uhai wake,Aurelia alikuwa mtu mwenye mawazo sana na alikuwa amejidhuru.

''Ninahisi nimefungwa mwilini mwangu, kichwani kwangu, ninataka kuwa huru,'' alisema

Aurelia Brouwers anasema alikuwa anaamini kuwa anaweza kufanya maamuzi.Lakini je kutamani kwake kufa ilikuwa dalili ya matatizo ya akili?

Haki miliki ya picha RTL Nieuws, Sander Paulus
Image caption Aurelia Brouwers akiwa ziwani karibu na makazi yake

''Nitajuaje-mtu atajuaje kuwa shauku yake ya kufa haikuwa dalili za matatizo ya akili? Daktari anasema kuwa watu hawa wamepoteza matumaini,lakini unaweza kuwasaidia kuwapa matumaini na unaweza kuwaonyesha kuwa huwezi kuwaacha.

Haki miliki ya picha RTL Nieuws, Sander Paulus
Image caption Aurelia Brouwers alipokuwa mtoto

.

Kifo cha mwanadada huyu kulizusha mjadala mkali nchini Uholanzi, na kushika vichwa vya habari duniani kote, hakuna aliyesema kuwa ilikuwa kinyume cha sheria, ingawa wakosoaji walihoji kama ni kesi ambayo bunge la mwaka 2002 lilipitisha ukatishaji wa maisha

Maoni yalikuwa tofauti kama kulikuwa kuna namna nyingine inayokubalika kumuokoa Aurelia.Kwa mfano Daktari Kit Vanmechelen anasema kuwa watu wanapoomba kutolewa uhai kutokana na matatizo ya akili, mara kadhaa hujiua wenyewe ikiwa maombi yao yatakataliwa

''Nimewatibu wagonjwa ambao nilijua watajiua,'' alieleza.''Nilijua .Waliniambia, nilihisi na nilifikiri,'Siwezi kukusaidia'.Hivyo kukatisha uhai ni njia ambayo nashukuru iko kwenye sheria.Wale ambao wanaweza kutoa uhai wao ninawaweka kwenye kundi la wagonjwa ambao watapoteza uhai wao.

Haki miliki ya picha RTL Nieuws, Sander Paulus
Image caption Manunuzi yake ya mwisho ya chakula

Aurelia Brouwers alikufa zaidi ya muongo mmoja kabla ya kufikia miaka 40 .Siku yake ya mwisho kuishi alitembelewa na mwanamuziki anayempenda sana, Marco Borsato.Usiku huo, alikula chakula cha usiku na marafiki zake-kulikuwa na vicheko.Asubuhi ya tarehe 26 mwezi Januari aliandika kwenye mtandao wa kijamii kwa mara ya mwisho.

''Ninajiandaa kwa safari yangu sasa.Asante sana kwa kila kitu.Sitapatikana tena kuanzia sasa''.

Wapendwa wake walijikusanya kwenye chumba chake, sambamba na madaktari wawili

Aurelia hakupewa dawa zilizomuua na madaktari, alizimeza dawa mwenyewe.

Alimwambia rafiki yake Sander Paulus akiwa ameshika chupa ya dawa iliyokuwa imefungwa

''Hii ni dawa'', alisema ''Ninajua ni chungu, hivyo nitakunywa kisha nilale''.

Sander alimuuliza kama ana mashaka yoyote

''Sina mashaka'', Aurelia alisema .''Niko tayari -tayari kufanya safari''.

Ninatumaini utakipata unachokitafuta, alisema Sander.

''Hakika ndivyo,'' Aurelia alijibu.

Aurelia aligeuka na kumwelekezea mgongo Sander Paulus, kisha alipanda ngazi.Ni muda wa baada ya nane mchana, siku ya Ijumaa,tarehe 26 mwezi Januari, 2018

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii