Korea Kaskazini: Kim Jong-un abaki na nguo ya ndani

Gazeti la Serikali Rodong Sinmun likimuonyesha mke wa Kim, Ri Sol-ju akiwa ameshika shati la mumewe Haki miliki ya picha Rodong Sinmun
Image caption Gazeti la Serikali Rodong Sinmun likimuonyesha mke wa Kim, Ri Sol-ju akiwa ameshika shati la mumewe

Picha mpya zilizotolewa na vyombo vya habari vya Korea Kaskazini zinamuonyesha Kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un akiwa amevua shati akibaki na nguo ya ndani , alipokuwa ametembelea kiwanda cha usindikaji samaki

Picha hizo , ambazo zilijaza kurasa mbili za kwanza za Gazeti la Serikali Rodong Sinmn, zinamuonyehsa kiongozi huyo akikagua kiwanda cha samaki

Si tu mtindo wake wa mavazi ulioeleza hadithi ya wenye nacho na wasionacho nchini Korea Kaskazini, lakini muda ambao ziara hiyo imefanyika unaonyesha namna pyongyang inavyoshughulikia changamoto ya chakula na joto kali mashariki mwa bara Asia.

Haki miliki ya picha KCNA
Image caption Kim Jong-un akijadiliana na maafisa kuhusu usindikaji wa samaki

Bwana Kim aliwasili akiwa amevalia shati la rangi ya kijivu, kofia pana na suruali pana.

Kwa Picha: Kusalimiana kwa Trump na Kim Jong Un na maana

Kutokana na hali ya hewa ya joto kali iliyofikia 37.8, aliamua kulivua shati lake na kuendelea na ukaguzi wake akiwa na nguo ya ndani akiwa ameichomekea kwenye suruali yake ya kijivu.

Lakini wakati kiongozi huyo akipata akipozwa na namna hii ya nguo, maafisa wake wengine wakiwemo maafisa wa kijeshi na viongozi wa kiwanda walibaki katika sare zao.

Mke wa Rais, Ri Sol-ju alionekana akiwa amebeba shati la mumewe.

Haki miliki ya picha KCNA
Image caption Kila mtu alikuwa ameloa maji kwenye kwenye shamba la samaki
Haki miliki ya picha KCNA
Image caption Ziara ya Kim katika kiwanda cha bidhaa za vilainishi mwaka 2014

Ziara mbili katika kipindi kisichozidi juma moja katika kiwanda cha samaki zinaeleza namna ambavyo Korea Kaskazini inavyopambana na joto kali.

Nchi hiyo imesema inakabiliwa na ukamekutokana na majira marefu ya joto kalli, hivyo huenda hali hiyo ikaathiri kilimo kwa kiasi kikubwa katika nchi hiyo ambayo imeripotiwa mwaka jana kuwa 70% ya watu wanategemea msaada wa chakula.

Hivyo ziara hii ni kuonyesha kuwa nchi hiyo imelenga kupata mbadala wa changamoto hiyo hasa kwenye samaki na uyoga.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii