Joto kali: Ng'ombe wazua vioja baada ya kutembelea fukwe za utupu Sweden

Ng'ombe wakiwa ufukweni wakitazama mtu akiogelea
Maelezo ya picha,

Ng'ombe wakiwa ufukweni

Serikali kusini mwa Sweden imetoa ruhusa kwa Ng'ombe kutembelea fukwe ambazo watu huzitembelea wakiwa watupu wakati wa majira ya joto, ingawa kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa watu katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa mitandao ya habari, watu wanaotembelea maeneo hayo wamekuwa wakiwalalamikia maafisa katika jimbo la Smaland kuhusu mifugo hiyo kutembelea fukwe zao, kuwa uwepo wao ni hatari kwa afya za binaadamu.

Vyombo vya habari vimesema majira hayo ya joto yamekuwa yakiathiri maeneo ya bara la Ulaya, yamesabisha kuwa na ukame nchini humo, na wafugaji wamekuwa katika wakati mgumu kuwalisha wanyama wao.

Hii inamaanishja kuwa baadhi ya wafugaji wameamua kuwachinja Ng'ombe wao mapema kuliko kawaida: lakini wengine walilazimika kupeleka mifugo kwenye fukwe, ili kuwapooza.

''Wakati kukiwa na ukame, huwezi kuwachinja tu bila sababu, wanahitaji kuoga, kula na kunywa,'' alieleza afisa wa manispaa Peter Bengtsson.

Bwana Bengtsson anasema wanaoogelea hawawezi kupata madhara kama vijidudu vya E.Coli, lakini wafugaji lazima waache kuwapeleka ng'ombe kwenye maji kama kuna watu ambao wanataka kuogelea.

Ameeleza kuwa ndege pia hutembelea fukwe hizo, lakini kama wameeleza kuwa hatarini kupata uzio au usalama wa afya zao uko mashakani, maafisa sharti wazungumze na wamiliki wa wanyama hao.