Mfanyakazi aiba ndege ya abiria na kuiangusha Seattle Marekani

A Horizon Air Bombardier Dash 8 Q400, reported to be hijacked, flies over Fircrest, Washington, the U.S., before crashing in the South Puget Sound, Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ndege iliyoibwa ikizunguka angania

Mfanyakazi mmoja wa shirika la ndege ameiba ndege isiyo na abiria kutoka uwanja wa ndege wa Seattle na kuiangusha karibu na kisiwa kilicho karibu.

Mamlaka zinasema kuwa mwanamume huyo alipaa na ndege hiyo bila ruhusa siku ya Ijumaa usiku saa za Marekani na kusababisha uwanja wa ndege kufungwa.

Ndege mbili za jeshi za F15 ziliifuata ndege hito. Haijulikani ikiwa mwanamume huyo alinusurika baada ya ndege hiyo kuanguka.

Haki miliki ya picha CBS
Image caption Picha za moto mahala ndege hiyo ilianguka

Polisi mkuu kaunti ya Pierce alisema kuwa hicho sio kitendo cha kigaidi akiongeza kuwa mwanamume huyo ni wa eneo hilo mwenye miaka 29

Waelekezi wa ndege walijaribu kumshawishi mwanamume huyo kutua kabla ndege hiyo kuanguka.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Abiria kwenye uwanja wa Seattle baada ya ndege kuibwa

Ndege hiyo ilikuwa aiana ya Horizon Air Q400, kwa mujibu wa taarifa ya shirika, mshirika wa Horizon la Alaska Airlines. Ilianguka kusini mwa kisiwa cha Ketron karibu na kituo cha kijeshi.

Kwenye kanda moja ya video mwanamume huyo anaweza kusikika akiwa na wasi wasi kuhusu ni kiasi gani cha mafuta alikuwa nacho. Pia alisema kuwa angetua mwenyewe kwa sababu alikuwa anafahamu kupitia michezo ya kompiuta.

Image caption Seattle

Mada zinazohusiana