Nasa yasitisha shughuli ya kutuma chombo kwenda kwa Jua

Artwork: Parker Solar Probe Haki miliki ya picha NASA-JHU-APL
Image caption Sasa chombo hicho kinatarajiwa kurushwa kikiwa kwenye roketi kubwa ya Delta-IV kesho Jumapili.

Shirika la anga la Marekani Nasa limehairisha shughuli ya kutuma chombo cha Satelaiti karibu na jua kuliko hapo awali.

Chombo hicho kinachojulikana kama Parker Solar Probe kilitarajiwa kuzinduliwa eneo la Cape Canaveral, Florida leo Jumamosi lakini uchunguzi wa dakika za mwisho umesababisha safari hiyo kuhairishwa.

Sasa chombo hicho kinatarajiwa kurushwa kikiwa kwenye roketi kubwa ya Delta-IV kesho Jumapili.

Satelaiti hii inatarajiwa kuwa chombo chenye kasi kubwa kuwai kutengenezwa na binadamu katika historia.

Haki miliki ya picha NASA
Image caption Parker kikiundwa

Roketi ilikuwa tayari eno la kuzindua wakati shughuli hiyo ilisimamishwa huku maafisa wakichunguza chanzo cha kengele kilicholia.

Satelaiti hiyo inatajwa kusafiri mbali angani eneo linalojulikana kama Corona.

Data zake zinatarajiwa kufichua siri kuhusu Jua yakiwemo matumaini kuwa itastahimili joto la juu zaidi la nyuzi 1,000 kutoka kwa jua.

Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Sasa chombo hicho kinatarajiwa kurushwa kikiwa kwenye roketi kubwa ya Delta-IV kesho Jumapili.

Roketi hiyo ya Delta itaipeleka satelaiti anga za mbali ili iweze kupita sayari ya Venus kwa kipindi cha wiki sita zijazo kabla iendelee na safari yake kwenda kwa Jua kwa muda wa wiki zingine sita.

Katika kipindi cha miaka saba Parker itazunguka mara 24 kwa Chua ikijaribu kusoma fisikia ya corona, eneo ambalo shughuli nyingi zinaoathiri dunia hutokea.

Chombo hiki kitangia ndani ya anga na kukaribia kwa kilomita milioni 6.16 kutoka kwa Jua lenye joto la juu kupindukia.

Kitakuwa chombo chenye kasi ya juu zaidi kuwai kuundwa na binadamu kikiwa na kasi ya kilomita 690,000 kwa saa.

Haki miliki ya picha MaX ALEXANDER/UKSA
Image caption Sasa chombo hicho kinatarajiwa kurushwa kikiwa kwenye roketi kubwa ya Delta-IV kesho Jumapili.