Kunguru werefu wanaokusanya taka kuanza kutumiwa Ufaransa

A rook crow Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kunguru wa kwanza tayari wameanza kufanya kazi huku wengine wakitarajiwa kujiunga nao siku ya Jumatatu.

Bustani moja nchini Ufaransa inatarajiwa kutumia kunguru sita werefu kukusanya taka na kusafisha eneo hilo.

Kunguru hao kwenye bustani ya Puy du Fou theme park magharibi mwa nchi wamefunzwa kukusanya mabaki ya sigara na taka zingine ndogo ndogo.

Kisha wanaweka taka hizo kwenye kisanduku kidogo, kisanduka ambacho baadaye hutumiwa kuwapa chakula kama njia ya kuwashukuru.

Kunguru wa kwanza tayari wameanza kufanya kazi huku wengine wakitarajiwa kujiunga nao siku ya Jumatatu.

Hii sio mara ya kwanza kunguru wameonyesha uerefu wao, mapema mwaka huu wanasayansi waliunda mashine ambayo ilionyesha uwezo wa kunguru kutatua masuala fulani.

Mashine hiyo ilihitaji karatasi yenye ukubwa fulani kuwe kusuluhisha jambo.

Wanasayansi waligundua kuwa kunguru wanaweza kukumbuka ukubwa wa karatasi hiyo na hata wangeikata na kuipindua kama haingeweza kutoshea kwenye mashine.

Mada zinazohusiana