Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 12.08.2018

Eden Hazard

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji,Eden Hazard

Klabu ya Real Madrid inajiandaa kutoa kiasi cha paundi za uingereza milioni 200 kwaajili ya kumnasa mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji Eden Hazard. (Express).

Real Madrid pia inalenga kumsajili kiungo mchezeshaji wa kimataifa wa Denmark na klabu ya Tottenham ya Uingereza, Christian Eriksen, ikiwa kiungo wake mwenye umri wa miaka 32 raia wa Croatia Luka Mondric ataamua kuondoka kujiunga na Inter Milan. (Sun)

Mlinda mlango wa klabu wa Atletico Madrid Jan Oblakm mwenye umri wa miaka 25 amekataa kujiunga na klabu ya Chelsea licha ya timu hiyo kufikia dau la kuvunja kipengele cha mkataba wake cha paundi milioni 90. (sunday Times)

Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji Riberto Martinez na msaidizi wake Thierry Henry wamo kwenye orodha ya kuziba nafasi ya kocha wa klabu ya Leicester City Claude Puel ambaye ana mechi mbili za kunusuru kibarua chake. (Sunday Mirror).

Beki wa kushoto wa klabu ya Leicester City ben Chilwell mwenye umri wa miaka 21, amesema mchezaji mwenzake raia wa Uingereza Harry Maguire aliyekuwa akihusishwa na kuhamia kwenye klabu ya Manchester United, atasalia kwenye timu yake mpaka mwishoni mwa msimu na hata ondoka kwenye dirisha la usajili la mwezi January. (Daily Star on Sunday).

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kocha wa klabu ya Arsenal Unai Emery

Kocha wa klabu ya Arsenal Unai Emery amemwambia mshambuliaji wake Danny Welbeck mwenye umri wa miaka 27 hivi sasa anataka kuona akifunga magoli mengi na kuisaidia timu wakati anapokuwa kwenye lango la wapinzani wake. (Telegraph).

Beki wa kati wa klabu ya Beyern Munich ya Ujerumani Jerome Boateng anatarajiwa kujiunga na klabu ya Paris St-Germain ya Ufaransa. (Abendzeitung in German).

Klabu ya PSG ya Ufaransa imeonesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 21, Ousmane Dembele. (Mundo Deportivo in Spanish).

Kocha wa klabu ya Barcelona Ernesto Valverde amesema hatarajii kuona mchezaji wake hata mmoja akiondoka kwenye klabu yake. (AS in Spanish).

Timu ya Manchester United inatarajiwa kumtangaza mkurugenzi mpya wa ufundi kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo. (Guardian).

Klabu ya Valencia ya Hispania inakaribia kufikia makubaliano ya kupata saini ya mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayekipiga na klabu ya PSG, Goncalo Guedes. (ESPN).

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Timu ya Real Madrid

Klabu ya Real Madrid inafikiria kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wake kinda raia wa Norway Martin Odegaard mwenye umri wa miaka 19 kwenda kujiunga na klabu za daraja la pili ili kuendeleza kipaji chake. (Sunday Mirror).

Beki wa zamani wa klabu ya Swansea raia wa Hispania, Angel Rangel mwenye umri wa miaka 35 anajiandaa kujiunga kwa mkopo na klabu ya QPR akiwa mchezaji huru. (Sun).

Kiungo wa kimataifa wa Uswis na klabu ya West Ham Edimilson Fernandes anajiandaa kujiunga na klabu ya Fiorentina kwa mkopo. (Express)

Mlinda mlango wa kimataifa wa Colombia mwenye umri wa miaka 29 David Ospina anajiandaa kuondoka kwenye klabu yake ya Arsenal na kwenda kujiunga na Besiktas lakini hata hivyo kumekuwa na wasiwasi wa makubalianon kufikiwa. (Sabah via Mirror)

Kocha wa klabu wa Bournemouth Eddie Howe amesema hakukuwa na mgogoro wowote katiak suala la hatma ya kiungo wake wa kimataifa wa Uingereza Harry Arteta ili ajiunge na klabu ya Cardiff. (Bournemouth Echo).

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa kimataia wa Ureno na klabu ya Juventus Christiano Ronaldo

Mshambuliaji wa kimataia wa Ureno na klabu ya Juventus Christiano Ronaldo amesema kuchangilia kwake golo alilofunga kwa kichwa akiwa na klabu yake ya zamani ya Real Madrid dhidi ya Juventus mjini Turini msimu uliopita lilimsaidia kujiunga na klabu hiyo msimu huu. (Mail).

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa klabu ya Flamengo na timu ya taifa ya Peru Paolo Guerrero

Mshambuliaji wa klabu ya Flamengo na timu ya taifa ya Peru Paolo Guerrero anakaribia kufuata nyayo za mbrazil mwenzake kwa kujiunga na klabu ya Internacional licha ya adhabu ya kufungiwa kwa kutumia dawa za kusisimua misuli. (Goal)

Kiungo wa klabu ya Ipswich na timu ya taifa ya Uingereza Andre Dozzell anajiandaa kuondoka klabuni hapo lwa mkopo. (East Anglian Daily Times).

Mlinda mlango wa klabu ya Liverpool mwenye umri wa miaka 30 ambaye pia ni kopa wa akiba wa timu ya taifa ya Ubelgiji Simon Mignolet anasubiri kupewa ofa nyingine kutoka kwa klabu ya Napoli ya Italia, amesema wakala wa mchezaji huyo. (Liverpool Echo, via Radio Kiss Kiss Napoli)