Mtalii kutoka China auawa na kiboko akipiga picha katika ziwa Naivasha Kenya

Picha yamponza mtalii
Maelezo ya picha,

Picha yamponza mtalii na kupoteza maisha yake Naivasha

Mtalii kutoka China, Chang Ming Chuang mwenye umri wa miaka 66 amefariki baada ya kuvamiwa na kiboko Jumamosi jioni.

Mamlaka ya hifadhi ya wanyama pori ya Kenya imeandika kwenye mtandao wake wa Twitter kuwa raia huyo kutoka China alivamiwa na kiboko wakati alipokuwa anampiga picha katika ziwa Naivasha eneo la sopa resort huko Nakuru.

Huku mwenzie Wu Peng Te mwenye umri wa miaka 62 amenusurika lakini bado yupo hospitali kwa ajili ya matibabu.

Kiboko huyo bado anatafutwa.