Mpiga picha mwanamke apinga vikwazo vilivyowekwa katika timu za mpira Iran

picha Haki miliki ya picha ABOLFAZL AMANOLLAH
Image caption Picha za mpiga picha mwanamke kutoka Irani akipiga picha mechi ya mpira akiwa mbali zasambaa mtandaoni

Mpiga picha wa Iran ameishangaza dunia baada ya kupinga vikwazo vinavyozuia wanawake kutoa taarifa za matukio ya michezo ya wanaume.

Parisa Pourtaherian, mwenye umri wa miaka 26, alishindwa kuingia katika dimba la Vatan Kaskazini mwa Iran kuripoti mchezo wa mpira wa miguu mwezi uliopita.

Dada huyo aliamua kutumia paa la nyumba ya jirani ya uwanja huo wa mpiga kwa kupiga picha kwa kamera yenye lenzi kali.

Licha ya kwamba hakuna tamko rasmi linalowakataza wanawake kuingia katika matukio ya michezo ila ni nadra kwa wao kuhudhuria kwa sababu mara nyingi huwa wanazuiwa kuingia.

Haki miliki ya picha PARISA POURTAHERIAN
Image caption Bi.Parisa alitumia paa ya nyumba ya jirani ya kiwanja cha mpira

Watu wengi wamemsifia bi. Pourtaherian kwa uamuzi wake wa kuripoti mechi ambayo alizuiliwa.

Parisa Pourtaherian aliisimulia BBC jinsi hali ilivyokuwa ;

"Nilifika kwenye uwanja wa mpira saa tatu kabla na lengo langu lilikuwa ni kupata nafasi ya kuniwezesha kupiga picha vizuri.Nilitafuta jengo la karibu ambalo lingeniwezesha kupiga picha lakini sikupata lolote kila mlango niliyopiga hodi sikufanikiwa.

Haki miliki ya picha PARISA POURTAHERIAN
Image caption Mwanamke alipiga hizi picha hizi licha ya katazo lililopo nchini mwake

Nilidhamiria kutokasirika hivyo hata kama ningeshindwa kufanikiwa nisingekasirika.Kwa sababu nilijua kama ningekasirika nisingeweza kupata fursa hii.

Katika kipindi cha mwisho cha michuano ile ,nilifanikiwa kumshawishi mmiliki wa nyumba ya jirani kuniruhusu kwenda kwenye paa ya nyumba yake.

Haki miliki ya picha PARISA POURTAHERIAN
Image caption Picha iliyopigwa na bi Parisa

Niliweza kufanya kazi yangu kwa kipindi chote cha pili ingawa iliniwia vigumu kuona sehemu moja ya uwanja kwa sababu kulikuwa na miti mbele yangu.

Nilikuwa siogopi ingawa polisi waliniona usiku ule wakati nafanya kazi yangu lakini hawakunifanya chochote na kuniacha niendelee na kazi yangu.

Nilipata faraja sana kupiga picha katika mechi iliyokuwa katika kiwango cha juu Iran haswa katika hali ya namna ile.

Wakati mpira ukiendelea na mimi nilikuwa naendelea na kazi yangu lakini wapiga picha karibu wote walikuwa wanapiga picha michuano hiyo walivutiwa kunipiga picha na mimi pia katika paa .

Niliweza kuziona picha zangu kwenye mitandao kadhaa ya kijamii na nyingine nilitumiwa na marafiki zangu.

Niliona hata muitikio wa watu wa Iran ulikuwa chanya na kunifanya kupata nguvu zaidi .

Haki miliki ya picha PARISA POURTAHERIAN
Image caption Mpira wa kikapu huwa wapiga picha wa kike hawakatazwi kama ilivyo mpira wa miguu

Ninapenda mpira wa miguu na ndio maana niliamua kuwa mpiga picha wa michezo.Huwa nnapiga picha zaidi katika michuano ya mpira wa wavu kwa sababu Iran kuna marufuku katika mpira wa miguu zaidi kuliko michezo mingine.

Ndoto yangu ni siku moja niweze kupiga picha mechi Manchester United katika uwanja wa Old Trafford.

Napenda kuwa mpiga picha ambaye nitaweza kusafiri katika maeneo mbalimbali kupiga picha katika michuano ya kimataifa.

Ila ndoto yangu kuu ni kuona wanawake wanapewa fursa sawa na wanaume wanapoenda kwenye mechi za mpira wa miguu."

Mada zinazohusiana