Kanye West akanusha kupagawa wakati alipoulizwa swali kuhusu Trump

Marekani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mwanamuziki Kanye West akiwa na rais Donald Trump wa Marekani

Mwanamuziki Kanye West amekanusha kupagawa wakati alipoulizwa swali kwenye kituo kimoja cha runinga kuhusu msaada aliotoa kwa rais Donald Trump na kusema kuwa hakuwa amepewa muda wa kujibu swali hilo.

Mwanamuziki huyo alionekana kutokuwa na jibu alipoulizwa kama anadhani kuwa rais Trump anajali maisha ya watu weusi au anajali maisha ya watu wote.

Ukimya wa mwanamuziki huyo wakati alipoulizwa swali juu ya rais Trump ndio uliosababisha mtangazaji kuweka tangazo la biashara .

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mwanamuziki wa hip pop Kanye West

Aidha Kanye West alidai kuwa hakuwa amepewa nafasi ya kujibu na ilikuwa ni muhimu kuchukua muda kufikiri kabla ya kujibu.

Mahojiano hayo yamezua mjadala dhidi ya mwanamuziki huyo wa miondoko ya kufoka mwenye umri wa miaka 41 ambaye awali alidai kuwa Trump ni kaka yake na wana nguvu zinazofanana.