Reli mpya ya SGR Kenya: Maafisa washtakiwa kwa madai ya ulaghai ya reli mpya ya SGR iliogharimu $3bn

Reli mpya ya SGR Kenya Haki miliki ya picha EPA
Image caption Reli hiyo mpya inaunganisha mji mkuu wa Nairobi hadi bandari ya Mombasa

Maafisa wawili wa serikali wameshtakiwa mahakamani kwa ulaghai kuhusu ujenzi wa reli mpya nchini Kenya kupitia ufadhili wa serikali ya China uliogharimu takriban $3.2bn (£2.5bn)

Wawili hao wameshtakiwa kwa kulipa $2m kama fidia kwa kampuni za kibinafsi zilizodai kumiliki ardhi ambayo reli hiyo ilipitia. Maafisa hao na wengine 15 wamepinga mashtaka hayo.

Reli hiyo ni mradi mkubwa tangu kupatikana kwa uhuru kutoka Uingereza 1963.

Rais Uhuru Kenyatta aliifungua mwezi Mei mwaka ulioipita, akisifu kuwa mwamko mpya katika historia ya Afrika mashariki.

Reli hiyo inapitia Mombasa na mji mkuu wa Nairobi , na ujenzi wake ulikamilishwa miezi 18 mapema zaidi.

Inatarajiwa kuunganisha Sudan Kusini , mashariki mwa DR Congo , Rwanda, Burundi na Ethiopia hadi bahari hindi.

Lakini mradi huo umekumbwa na madai ya ufisadi mbali na madai ya wanauchumi kwamba gharama yake ilikuwa ya juu mno.

Ilipata hasara ya $100m katika mwaka wake wa kwanza wa operesheni , kulingana na takwimu rasmi.

Mradi huo ulishutumiwa na mashirika ya wanyama pori kwa kuwa reli hiyo inapitia mbuga ya kitaifa ya Tsavo kusini mashariki mwa Kenya.

Mkuu wa shirika la reli nchini Kenya Atanas Maina na mwenyekiti wa tume ya ardhi nchini Kenya Muhammad Swazuri walishtakiwa kwa ulaghai siku ya Jumatatu kufuatia kukamtwa kwao siku ya Jumamosi.

Wakenya wengi wameunga mkono kukamatwa kwa wawili hao walioonekana kuwa 'wasiowezekana' kutokana na ushawishi wao wa kisiasa waliokuwa nao, kulingana na mwandishi wa BBC Ferdinand Omondi.

Waliwekwa pingu baada ya kukaa kizimbani katika mahakama ya Nairobi.

Wakurugenzi wa kampuni kadhaa ni miongoni mwa watu 17 waliotuhumiwa, ripoti hiyo imeongezea. Wote wamekataa mashtaka hayo.

Kukamatwa kwao ni ishara ya serikali kuimarisha kampeni kumaliza utamaduni wa ukiukaji wa sheria uliopo nchini Kenya ripota huyo amesema.

Serikali imevunjilia mbali majumba kadhaa muhimu mjini Nairobi katika kipindi cha wiki moja iliokwisha na mamia ya majumba mengine yamelengwa katika operesheni ya kukomboa ardhi za umma.

''Akizungumza katika ibada ya kanisani siku ya Jumapili rais Uhuru Kenyatta alisema kwamba katika kipindi cha wiki chache nimepoteza marafiki wengi. Nimepokea simu nyingi zikisema unawezaje kukaa na kutazama ubomoaji unaondelea .Lakini nilisema ni vigumu kusitisha sio kwamba tunapenda kuvunja bali kukabiliana na ukiukaji wa sheria''.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii