Vyakula visivyo vya wanga vinaweza kukupunguzia maisha kwa miaka minne

Vyakula vyenye mafuta Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Vyakula vyenye kiwango kidogo cha wanga vina mafuta na protini nyingi

Lishe yenye kiwango kidogo cha wanga inauwezo kupunguza kiwango cha maisha ya binadamu ya kuishi, Utafiti umebaini hilo.

Lishe yenye virutubisho kidogo vya wanga, kama vile Atkins imepata umaarufu zaidi kama njia bora ya kupunguza uzani na umeonyesha matokeo ya kudumu ya kupunguza hatari ya kupatwa na magonjwa mengine.

Lakini utafiti wa Marekani uliofanywa kwa zaidi ya miaka 25 umeonyesha kupunguza kwa matumizi ya wanga au Kabohaidret - au kutumia nyama badala ya protini na mafuta yanayotoka - kwa mimea ni bora zaidi kiafya.

Utafiti huo ulizingatia watu ambao waliokuwa wakifahamu kiwango cha Kabohaidreti walichokuwa wamebugia.

'Kupata umaarufu zaidi'

Katika utafiti uliofanywa na kuchapishwa kwenye jarida la kisayansi la afya la Lancet , watu 15, 400 kutoka Marekani walijaza hoja kuhusiana na chakula na vinywaji wanavyotumia na kwa kiwango gani.

Kutokana na utafiti huo , wanasayansi walikadiria kiwango cha Kalori watu hao hupata kutoka kwa vyakula vyenye proteini , mafuta na Kabohaidreti(vyakula vya wanga)

Baada ya kundi hilo ambalo liliwajumuisha watu wengi wenye kadri ya umri wa miaka 25, watafiti hao walibaini kwamba kati ya asilimia 50-55% hupata nguvu kutoka kwa vyakula vilivyo na wanga.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Vyakula aina hii zinauwezo wa kumafanya mtu kuzeeka katika hali nzuri

Vyakula vya wanga ni pamoja na mboga, matunda, sukari ambayo hutokana kwa vyakula vya mafuta kama vile viazi, mkate, wali , tambi na vyakula vya nafaka.

Watafiti hao wamekadiria kwamba watu wanapofika miaka 50 , katika kiwango cha watu wanaotumia Kabohaidreti katika hali ya wastani wanatarajiwa kuishi miaka 33 zaidi.

Utafiti huo ni sawa na utafiti wa hapo awali ambao waandishi walilinganisha utafiti iliyoliwajumuisha zaidi ya watu 400,000 katika zaidi ya nchi 20.

Wanasayansi walinganisha vyakula vyenye viwango vidogo vya kabohaidreti vinavyotoka kwa proteini inayotokana kwa wanyama .

Utafiti: baadhi ya vyakula husababisha ukomo wa hedhi mapema

Walibaini kwamba ulaji wa kiasi kikubwa wa nyama ya ng'ombe, nguruwe , kuku, kondoo na chizi au jibini badala ya kabohaidreti imehusishwa kwa kiwango kidogo cha kuongeza hatari ya mtu kufariki.

Lakini matumizi ya kutumia kabohaidreti badala ya mboga zenye protein na mafuta kama vile Maharagwe na jungu , zilibainika kupunguza hatari ya mtu kufariki mapema.

Je wajua kwamba mtoto akipewa chakula kigumu mapema analala vizuri?

Dkt. Sara Seidelmann wa kliniki ya utafiti kutoka Brigham na hospitali ya wanawake huko Boston aliyeongoza utafiti huo amesema lishe yenye kiwango kidogo cha kabohaidreti inayochukua nafasi ya Proteini na mafuta inazidi kupata umaarufu kama njia ya kiafya ya kupunguza uzani.

Hata hivyo, data imedhihirisha kwamba kabohaidreti zinazotokana na vyakula vinavyotoka kwa wanyama vinavyotumiwa sana kaskazini mwa Marekani na ulaya, vinahusishwa na muda mfupi wa kuishi na lazima watu wakatazwe.

''Licha ya iwapo mtu atahitaji kufuata mkondo huo wa kupunguza kiwango cha kabohaidreti na kutumia kabohaidreti zinazotokana na mimea inaweza kumuongezea maisha marefu yenye afya bora.''

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii