Kwa nini Trump anajenga kikosi kipya cha jeshi la anga za mbali?

A rocket is launched from the Vostochny Cosmodrome to deliver satellites

Chanzo cha picha, Getty Images

Marekani inataka kuunda jeshi la anga za mbali.

Wana anga hawatapewa silaha hivi karibuni lakini kulingana na makamu wa rais wa Marekani Mike Pence, ni kuwa China na Urusi wamekuwa wakiunda silaha za kushambulia setilaiti ambazo pia zinatakiwa kukabiliwa.

"Mazingira ya anga za mbali yamebadilika miaka iliyopita," alisema Pence wakati alikuwa akieleza kile kikosi hicho kipya kitafanya.

Alisema kutabuniwa kikosi cha jeshi ambacho kitakuwa na majukumu ya kulinda maslahi ya Marekani kama vile setilaiti zinazotumiwa kwa mawasiano na ujasusi.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

The space shuttle Discovery made its final mission to the International Space Station in 2011

Rais Trump ambaye aliuzungumzia mpango huo mapema mwaka huu alionya kuhusu hatua hizo za kijeshi zimechukuliwa na washindani wa Marekani.

Rais Alisema: "Nimeona vitu ambavyo hamngetaka hata kuviona."

Ni kwa nini Marekani ina wasi wasi?

Kuna huduma za kijeshi na za kiraia kwenye anga za mbali lakini wakati mwingine zinaweza kukutana.

Teknolojia ya mawasialio ya setilaiti inayofahamika kama Global Positioning System (GPS) ilianzishwa na jeshi la Marekani lakini baadaye iliruhusiwa kwa matumizi ya kiraia.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Roketi ya Urusi ya Soyuz TMA-19M ikibeba setilaiti

Anga za mbali zimekuwa zikitumiwa kwa masuala ya kijeshi tangu miaka ya sitini, anasema Alexandria Stickings

Wakati wa vita baridi Marekani na muungano wa usovieti hakuwa na vita kwenye anga za mbali lakini walitumia setilaiti kuchunguzana.

China, Urusi na Marekani wamefanyia majaribio salaha ambazo zina uwezo wa kuharibu setilaiti.

Haya ni makombora yanayoweza kurushwa kutoka duniani moja kwa moja kwenda kuigonga setilaiti kenye orbit.

Maelezo ya picha,

setilaiti zilizo angani

Hizi ni silaha zinazofahamika kama 'co-orbitals', ambazo ni setilaiti zilizotundikwa kwa makombora yanayorushwa kutoka duniani.

Setilaiti hizi kisha hujitoa kutoka kwa kombora na kuingia orbit kulenga setilaiti fulani kwa kuishika au kuigonga.

Pence alizungumzia kuongeza kwa silaha za China na Urusi katika anga za mbali.