Pete iliyopotea shambani miaka 12 iliyopita yapatikana kwenye karoti

Chanzo cha picha, Lin Keitch
Pete iliyopotea shambani miaka 12 iliyopita yapatikana kwenye karoti
Pete ya dhahabu ambayo ilipoptea kwenye shamba moja miaka 12 iliyopita umepotikana kwenye karoti iliyokuwa imevunwa kwa mapishi ya jioni.
Lin Keitch, 69, kutoka Monkton Heathfield karibu na Taunton aliipata pete hiyo wakati alikuwa akiosha mboga alizokuwa amevuna kutoka shamba lake ndogo.
Ilikuwa ni zawadi aliyopewa alipoifikisha umri wa miaka 40 kutoka kwa mumewe na ilipotezwa na binti yao.
Wawili hao wanaamini kuwa karoti hiyi ilikua kwennye pete, na Bi Keutchg amesema ni ugunduzi moja kwenye milioni.
"Mumewe wangu Dave ndiye alivuna karoti hizo na kisha akaziweka kwenye mlango wa nyuma," alisema.
Chanzo cha picha, Lin Keitch
Dave aliinunulia wakati mke wake alifikisha umri wa miaka 40
"Dave aliinunulia wakati nilifikisha umri wa miaka 40, lakini ikifika wakati hainitoshi nikampa binti yetu.
"Akaipoteza shambani, imepita miaka 12 tangu wakati huo. Nilifikiri sitaipata tena.
Dave Keitch, 69, alisema alikuwa ameitafuta pete hiyo kwa miaka kadhaa kila mara alipokuwa akifanya kazi shambani.
Hakugundua kuwa alikuwa ameivuna kwenye karoti wiki iliyopita.
Wakati Lin aliweka mboga kwa bakuli kundaa chakula cha jioni aliiona pete hiyo kwenye karoti, Anasema aliona furaha isiyoelezeka.