Hatua ya Putin kuhudhuria harusi ya waziri nchini Austria yazua malalamiko

Austrian Foreign Minister Karin Kneissl and Russian President Vladimir Putin dance during her wedding on 18 August 2018 in Gamlitz, Austria

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Putin alimpa mauaa na kecheza densi naye kwenye shetrehe hiyo iliyoandaliwa kwenye mkoa wa Kusini mwa Austria wa Styria.

Rais wa Urusi Vladimir amehudhuria sherehe ya harusi ya waziri wa mashauriya nchi za kigeni wa Austria Karin Kneissl ambaye amekosolewa kwa kumualika.

Putin alimpa mauaa na kecheza densi naye kwenye shetrehe hiyo iliyoandaliwa kwenye mkoa wa Kusini mwa Austria wa Styria.

Wanasiasa wa upinzani wamemlaumu Bi Kneissl kwa kuhujumu sera za kigeni za Ulaya kwa kumualika mgeni wake huyo.

Putin alisimama Austria akiwa njiani kwenda Ujerumani ambapo atafanya mazungumzo na Chansela wa Ujerumani Angela Merkel.

Bi Kneissl anafunga ndoa na mfanyabiashara Wolfgang Meilinger kwenye sherehe katika mji mdogo wa Gamlitz karibu na mpaka na slovenia.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Bw Putin alialikwa wakati alifanya ziara nchini Austria mapema mwaka huu.

Bi Kneissl msomi asiye na chama, aliteuliwa kuwa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni na chama cha mrengo wa kulia kilicho mshirika kwenye serikali ya sasa.

Bw Putin alialikwa wakati alifanya ziara nchini Austria mapema mwaka huu.

Kumekuwa na mjadala kwenye vyombo vya habari nchini Austria kuhusu kuwepo kwa rais Putin tangu itangazwe wiki iliyopita.

Baadhi ya wanasiasa wamelalamika kuhusu matumizi ya pesa za walipa kodi kuweka ulinzi eneo hilo.

Putin anatarajiwa kufanya mazungumnzo na chansela Merkel kuhusu masuala kadhaa.