Kwa nini Wakenya wameorodheshwa kuwa wahamiaji wenye bidii zaidi nchini Marekani?

New York, Marekani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

New York, Marekani

Wahamiaji kutoka nchini Kenya wanaofanya kazi nchini Marekani wameorodheshwa katika nafasi ya tatu kati wahamiaji wa kigeni wanaofanya kazi kwa bidii zaidi nchini humo.

Wafanyakazi wa Kenya walipata alama 73.4 kuchukua nafasi ya tatu miongoni mwa wafanyakazi wenye ujuzi zaidi na bidii nchini Marekani kwa mujibu wa ripoti ya Bloombeerg ya mwaka 2018

Utafiti huo unawaweka raia wa Ghaana katika nafasi ya kwanza na wale wa Bulgeria kwenye nafasi ya pili wakiwa na asilimia 75.2 na 74.2 mtawalia.

Nchi zingine za Afrika zinazotajwa katika orodha ya kumi bora ni Ethiopia nafasi ya nne, Misri nafasi ya tano, Nigeria nafasi ya nane na Liberia nafasi ya tisa.

Hii imefanya waafrika kwa jumla kuwa wahamiaji wenye mazao ya juu zaidi nchini Marekani mbele ya wale kutoka Mexico na Amerika ya kati wanaochukua asilimia 70 ya raia wa kigeni wanaoishi Marekani.

"Ikiwa tunataka wafanyakazi wenye ujuzi wa juu na wenye bidii wanozungumza lugha ya kiingereza sehemu bora ya kuelekea ni Afrika," mwandishi wa habari wa Bloombeerg, Justin Fox, ambaye aliandika ripoti hiyo alisema.

Ripoti hiyo iliyotokana na utafiti wa mwaka 2016 pia ilisema kuwa Kenya ni kati ya nchi za Afrika zina wahamiaji wengi zaidi wanaosoma na kufanya kazi nchini Marekani.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wafanyakazi wa Kenya walipata alama 73.4 kuchukua nafasi ya tatu miongoni mwa wafanyakazi wenye ujuzi zaidi na bidii nchini Marekani

Kulingana na ripoti hiyo Kenya, Ghana, Nigeria na Nepal zina raia wengi wanaosomea elimu ya juu nchini Marekani baada ya Saudi Arabia.

Ripoti hiyo ilisema kuwa idadi ya wakenya wanaoshi kihalali na kufanya kazi nchini Marekani kuwa 120,000

Ripoti hiyo inakuja miezi mitatatu baada ya utafiti wa Benki Kuu ya Kenya kuonyesha kuwa wakenya wanaoishi na kufanya kazi nchi za nje walituma dola milioni 645 kati ya mwezi Januari na Machi mwaka 2018.

Hili ni ongezeko la karibu asilimia 50 kutoka dola milioni 434 ambapo wakenya wanaoishi nje walituma nyumbani kipindi kama hicho mwaka 2017.

Licha ya hilo ripoti hiyo inakuja wakati utawala wa Trumpo unaendelea kuwasaka na kuwafukuza wahamiajia haramu wakiwemo Wakenya.

Mwaka uliOpita wakenya 100 walifukuZwa kutokA Marekani ikiwa ni ongezeko kubwa tangu Trump aingie madarakani tarehe 20 Januaria mwaka 2017.