Kijiji ambapo wanaume na wanawake huzungumza lugha tofauti Nigeria

By the age of 10 boys are expected to speak the 'male language.'
Maelezo ya picha,

Akifika umri wa miaka 10 watoto wa kiume wanastahili kuzungumza lugha ya wanaume

Ubang, jamii ya wakulima kusini mwa Nigeria, wanaume na wanawake wanasema kuwa wao huzungumza lugha tofauti. Wanataja tofauti hiyo kama baraka kutoka kwa Mungu lakini vijana wengi sasa wanatumia lugha ya kiingereza ambayo imepata umaarufu, kuna hofu kuwa huenda tamaduni hiyo haitadumu.

Akiwa amevaa nguo za rangi tofauti, Chifu Oliver Ibang anawaita watoto wake wawili, akiwa na nia ya kutofautisha kati ya lugha hizo mbili.

Anashika mhogo na kumuuliza binti yake hiki ni kitu gani?

"Ni irui," anajibu kwa haraka.

Lakini kwa jamii ya Ubang lugha inayotumiwa na wanaume kwa mhogo, moja ya vyakula kuu nchini Nigeria ni "itong".

Pia kuna mifano mingine kama jina la nguo ambalo ni "nki" kwa wanawake na "ariga" kwa wanaume.

Chanzo cha picha, BBC/Olaniyi Adebimpe

Maelezo ya picha,

Community members say the sexes understand each other but only use the language of their sex

Haifahamiki haswa ni maneno mangapi yana tofauti na hakuna mfumo kamili ikiwa maneno haya yanatumiwa sana au yana uhusiano wowote na wajibu wa wanaume na wanawake.

Kuna maneno mengi ambayo wanaume na wanawake hutumia kwa pamoja, lakini kuna mengine ambayo yana tofauti kabisa kulingana na jinsia. Maneno hayo yana tofauti kabisa, anasema mtaalamu mmoja Chi Chi Undie, ambaye aliifanyia utafiti jamii hiyo.

'Ishara ya ukomavu'

Anasema tofatu ni kubwa hata kuliko kwa mfano ya lugha ya kiingeza inayotumiwa Uingereza na Marekani.

Lakini wanawake na wanaume wanaelewana vyema.

Maelezo ya picha,

Chief Oliver Ibang anataka kujenga kituo cha lugha kuonyesha tamaduni ya Ubang

Hi ni kutokana na sababu kuwa watoto wa kiume hukua wakiwa wanazungumza lugha ya wanawake, kwa sababu wao hutumia muda wao mwingi wa utotoni wakiwa na mama zao na wanawake wengine, kulingana na chifu Ibang.

Afikapo umri wa miaka 10, mtoto wa kiume hutakiwa kuzumgumza lugha ya wanaume, anasema.

"Kuna wakati mtoto wa kiume hufika na kugundua kuwa hatumii lugha inayotakikana. Hakuna mtu wa kumwambia kuwa anahitaji kubadilisha lugha na kutumia lugha ya wanaume.

"Wakati anaanza kuzungumza lugha ya wanaume, sasa hapo utajua kuwa ameanza kukomaa."

Ikiwa mtoto hawezi kubadilisha na kuzungumza lugha sahihi umri fulani anatajwa kuwa aliye na matatizo ya akilia, anasema.

Maelezo ya picha,

Ubang is a tightly knit community steeped in tradition and custom

Watu wa Ubang wamajifunia sana lugha yao.

Lakini kuna maoni tofauti ni vipi lugha zikaja kuwa mbili. Wengi wanasema ni sababu za Kibiblia.

"Mungu aliwaumba Adamu la Hawa na wao walikuwa ni watu wa jamii ya Ubang," chifu anasema.

Mpango wa Mungu ulikuwa kuipa kila kabila lugha mbili, lakini baada ya kuumba lugha mbili kwa Ubang aligundua kuwa hakukuwa na lugha za kutosha za kuwapa wengine, anaeleza

Kwa hivyo aliwacha. Hivyo ndiyo Ubang walinufaika na lugha mbili, Tuna tofauti na watu wengine duniani.

Maelezo ya picha,

Uban Nigeria