Kwa nini msichana huyu kutoka Nigeria ni nyota wa teknolojia ya siku zijazo

Tomisin in a market in Ikeja
Maelezo ya picha,

Tomisin anatumai kwamba programu yake itawasaidia watoto waliopotea

Mwanafunzi Tomisin Ogunnubi ni kijana anayependa sana kutengeneza programu za kiteknolojia

Miaka mitatu iliyopita alitengeneza, programu ya My locator, inayowasaidia watoto waliopotea.

Programu hiyo ya simu ambayo inapatikana katika hifadhi ya Google tayari imeanza kupakuliwa zaidi ya mara 1000 tangu uzinduzi wake mwaka wa (elfu mbili na kumi na sita) 2016.

'Programu hiyo inaweza kukushirikisha na ramani ya Google na kukuonyesha maelezo ya mahali ulipo hadi katika eneo ulilohifadhi'', Tomisin ambaye sasa ana umri wa miaka 15 na anayesoma mjini Ikeja anaelezea.

Hatua za dharura

"Pia ina uwezo ambapo unapobofya kitufe cha dharura, inatuma ujumbe na kupiga simu -iwapo umeiwezesha hadi katika nambari uliopendelea".

"Inaweza kuwa nambari ya dharura ama nambari ya mtu wa familia. Ni chaguo lako. Hivyobasi iwapo kuna dharura, na unahitaji majibu ya haraka inatuma anwani yako kwa nambari hiyo ili mtu aweze kufahamu kwa haraka mahala ulipo''

"Nataka habari za haraka kuhusu usalama nikifikirie kwamba ….kuna watu hatari tofauti, hivyo basi nadhani wazo la kuweza kutoka nje na kuwa salama ndio lililonishinikiza kuanzisha programu hii", anaelezea.

Maelezo ya picha,

Programu ya Tomisin tayari imepakuliwa zaidi ya mara 1000

"Lakini nilikuwa na umri wa miaka 12 nikifikiria kuhusu wazo hilo, na sasa nimejifunza jinsi ya kutengeneza programu. Kwa nini basi nisitumie nilichojifunza kutengeneza kitu ambacho kinaweza kuwa na manufaa kwangu mimi na watu wengine?''

Aniedi Udo-Obong meneja wa programu katika kampuni ya Google anasema kuwa kuna uhaba wa watu wa kuenziwa katika sekta hiyo nchini Nigeria huku watu wengi nchini humo wakienzi watu kama vile Elon Musk na mark Zuckerberg.

"Lakini wanafunzi zaidi wa vyuo vikuu wameanza kutambua sekta hiyo kama njia nzuri ya kujipatia kipato kupitia kuanzisha kampuni za kiteknolojia", anaongeza kusema.

Maelezo ya picha,

Tomisin anaenziwa na wanafunzi wenye umri mdogo katika shule yake

Anedi mara kwa mara hukutana na wafanyibiashara wenye mawazo mengi katika kampuni ya Google. Kazi yake inashirikisha kuanzisha uhusiano na wavumbuzi ili kuimarisha mazingira Afrika. Anaelezea kwamba kuna haja ya kuimarisha programu ya my Locator , lakini anasema kuwa Tomisin tayari amepiga hatua muhimu.

"Ninafurahishwa na programu ya Tomisin kwa sababu mbili. Napendelea kuona bidhaa katika hali yoyote badala ya kusikia kuhusu wazo zuri zaidi. Napenda kusikia kwamba mtu amekuwa na wazo kichwani mwake na kuweza kulishughulikia na kukamilisha kitu'', anasema.

Vipaji vya vijana

Mwalimu wa Tomisin anayefunza somo la sayansi ya tarakilishi Kofoworola Cole anasema kuwa,ufanisi wa kijana huyo ulichangia pakubwa vile shule hiyo inavyofundisha somo hilo. Pia umechangia pakubwa katika kuwashinikiza wanafunzi katika shule hiyo.

''Ilitupatia motisha kuweza kuanza miongoni mwa watoto wenye umri wadogo, kawaida tuliwalenga wanafunzi wakubwa. Lakini wakati Tomisin alipofanikiwa tulijua kwamba ni kweli kuna vipaji katika madarasa yenye vijana wenye umri mdogo'', alisema

Aniedi anasema kuwa uwekezaji mkuu katika sekta ya elimu unahitajika ili kupunguza mwanya uliopo kati ya wanafunzi wanaotoka katika familia tajiri na wale wanaotoka katika jamii masikini.

Maelezo ya video,

Teknolojia yatumiwa kukabiliana na wasiolipa madeni Kenya

"Tumeona mipango inayolenga madarasa ya watoto wadogo katika shule za msingi katika mataifa megine kama vile Estonia, Uingereza, China na Korea…nina hofu kwamba huenda tukawachwa nyuma iwapo hatutawahusisha watoto wetu katika kiwango kama hicho wakiwa na vifaa na teknolojia ambazo wenzao katika mataifa mengine na masoko wanatumia kujifunza'', anasema.

"Teknolojia ndio tegemeo la siku zijazo na kuweza kujua teknolojia ndio kuweza kutatua matatizo'', anasema Tomisin

'' Ninapenda teknolojia kwa sababu kuweza kuleta mabadiliko ni kitu ninachopenda kufanya''.

Kipindi hiki cha BBC kiliandaliwa kupitia ufadhili wa wakfu wa Bill na Melinda gates.