Kwa nini msichana huyu kutoka Nigeria ni nyota wa teknolojia ya siku zijazo

Kwa nini msichana huyu kutoka Nigeria ni nyota wa teknolojia ya siku zijazo

Mwanafunzi Tomisin Ogunnubi ni kijana anayependa sana kutengeneza programu za kiteknolojia.

Miaka mitatu iliyopita alitengeneza, programu ya My locator, inayowasaidia watoto waliopotea.

Programu hiyo ya simu ambayo inapatikana katika hifadhi ya Google tayari imeanza kupakuliwa zaidi ya mara 1000 tangu uzinduzi wake mwaka wa (elfu mbili na kumi na sita) 2016.