Naibu Jaji mkuu wa Kenya Philomena Mwilu akamatwa kwa tuhuma za ufisadi

Naibu Jaji mkuu Kenya Philomena Mwilu (Katikati)

Chanzo cha picha, YASUYOSHI CHIBA

Maelezo ya picha,

Naibu Jaji mkuu Kenya Philomena Mwilu (Katikati)

Naibu Jaji mkuu Kenya Philomena Mwilu amekamatwa na kushtakiwa kwa uhalifu katika mahakama mjini Nairobi.

Amekabiliwa na mashtaka ya kutumia vibaya mamlaka, na kukwepa kulipa ushuru.

ameachiliwa kwa dhamana ya thamani ya $50,000 na anatarajiwa kufika mahakamani Jumatano asubuhi.

Awali Mwilu alipelekwa katika makao ya idara ya uchunguzi wa uhalifu DCI kuhojiwa.

Ni kiongozi wa juu katika idara ya mahakama kuwahi kukamatwa katika operesheni ya serikali kukabiliana na rushwa nchini.

Muda mfupi baada ya kukamatwa, mwendesha mashtaka mkuu nchini Noordin Haji ameitisha mkutano wa dharura na waandishi wa habari kuhusu suala hilo.

Haji ameeleza kwamba idara ya mahakama itafanya kazi tu iwapo maafisa wa mahakama watatumia nafasi zao kujitajirisha kwa kisingizio cha Wakenya.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, mwendesha mashtaka huyo ametaja kuwa kuna ushahidi wa kutosha kumshtaki Mwilu kwa mkosa yakiwemo kutumia vibaya mamlaka kujinufaisha binafsi.

Maelezo ya picha,

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Bw Noordin Haji

Inaarifiwa kwamba Mwilu alikamatwa baada ya msururu wa mikutano ya tume ya huduma za mahakama, leo asubuhi.

Ni mara ya kwanza katika hostoria ya Kenya kukamatwa kwa kiongozi wa juu wa idara ya mahakama inayotokana na uchunguzi na kampeni ya serikali kupambana na rushwa nchini.

Chanzo cha picha, AFP/GETTY

Maelezo ya picha,

Mkurugenzi Mkuu wa NYS Richard Ndubai akiwa mahakamani

Kampeni ya serikali kupambana na rushwa:

Ahadi kuu ya Rais Uhuru Kenyatta alipochaguliwa kwanza kuingia uongozini mnamo 2013 ilikuwa ni kupambana na rushwa.

Lakini wakosoaji wake wanaeleza kwamba kasi haijaridhisha ya kulishughulikia hilo.

Kwa muda mrefu wengi wanataja kwamba kuwakamata viongozi wajuu serikali wanaotuhumiwa kuhusika na rushwa ndio njia pekee ya kuondosha ukwepaji wa sheria

Mnamo 2016, Kenya ilielezwa kupoteza thuluthi moja ya bajeti yake ya serikali kutokana na rushwa kila mwaka.

Licha ya kwamba hatua kama hii ya kukamatwa kwa maafisa wa ngazi ya juu serikali ambayo inatazamwa kuwa ya kutotarajiwa katika kihistoria ya Kenya, baadhi wanaona kwamba hatua hii sio ya kushangaza.

Kumeshuhudiwa visa kadhaa vya maafisa wa serikali kukamatwa kutokana na kutuhumiwa katika kashfa za rushwa lakini hakuna aliyehukumiwa kufikia sasa.

Hatahivyo uchunguzi wa hivi karibuni na kesi zilizowasilishwa dhidi ya maafisa wakuu baadhi zinaoenakana kuwa na nafasi ya kubadili mtazamo wa vita hivyo nchini tangu kuwepo kwa rushwa ya Anglo Leasing.

Maelezo ya picha,

Raia wa kenya wameiambia BBC kuwa wamechoshwa kuachiliwa huru kwa watu wanaopora pesa zao

Kufikia sasa, serikali imewakama washukiwa wanaotuhumiwa kuhusika katika wizi wa takriban dola milioni 100 katika kashfa ya shirika la kitaifa la huduma kwa vijana .

Mkuu wa shirika hilo alifikishwa mahakamani pamoja na washukiwa wengine wakuu katika kashfa hiyo mnamo Mei mwaka huu katika hatua ilio ya nadra ya kuwawajibisha maafisa wa serikali.

Wakenya wengi wanasema wanaamini kwamba kashfa hiyo inagharimu sehemu tu ya fedha zinazotuhumiwa kuibwa nchini kila mwaka.

Kwa sasa kuna ridhaa na hisia ya kuunga mkono hatua hii ya sasa na wito uliopo ni kwamba kiongozi wa taifa asiteteleke wakati serikali inapochukua hatua dhidi ya rushwa nchini.