Kondomu zinazolinda mawasiliano kwa wavuvi
Huwezi kusikiliza tena

Wavuvi watumia kondomu kulinda simu zao baharini pwani Kenya

Wavuvi kutoka pwani ya Kenya huko mjini Mombasa wamebuni mbinu mpya ya kulinda mawasiliano yao katika bahari ya Hindi. Wameanza kutumia mipira ya kondomu ili kulinda simu zao za mkononi , swala ambalo limewashangaza wengi. Hatua hiyo imerahisisha mawasiliano yao na wenzao walio nchi kavu iwapo kuna hatari yoyote mbali na wateja wao.