Ninatapika mara 30 kwa siku - tatizo la kiafya linalomkumba mwanamke wa miaka 19

Caitlin White
Maelezo ya picha,

Caitlin White, 19, anaugua hali inayojulikana kama gastroparesis

Kijana mmoja mwenye tatizo la tumbo lisilo la kawaida ambalo husababisha atapike hadi mara 30 kwa siku anelezea hali ngumu anayopitia.

Caitlin White, 19, kutoka Perth, anakumbwa na hali inayofahamika kama gastroparesis.

Matibabu yake kwa sasa ni pamoja na kulazimishwa kutapika kila siku shughuli ambayo huchukua hadi saa 12.

Tatizo analokumbana nalo ni kuwa ikiwa atachelewa kusafisha tumbo lake ataanza kutapika kila mara.

Athari zingine zinazomkumba ni kwa mfano ile huambia mwili wake kuwa mgonjwa.

Safari hospitalini

Akihojiwa na BBC Scotland Caitlin alisema, "maisha yangu ya kila siku ni safari za kwenda hospitalini.

"Ninaenda hosptalini kila siku kupima damu yangu na kulazimisha kutapika shughuli ambayo inaweza kuchukua masaa manne hadi nane.

Chanzo cha picha, Caitlin White

Maelezo ya picha,

Akiwa mtoto hakuwa na hali hii lakini mara ya kwanza aliugua akiwa na miaka 14

"Siku zingine inaweza kudumu saa 12, vile ilivyokuwa hiyo jana yaani Jumapili.

"Siruhusiwi kuendesha gari kwa sababu ya hali yangu. Niko na hali inayojulikana kama postural tachycardia syndrome, kwa hivyo mpigo wangu wa moyo huwa wa kasi."

Cailtin mara ya kwanza alikuwa mgonjwa na hali hii akiwa na miaka 14.

Kwa sasa na uzani wa kilo 38.

Katika kipindi cha miaka mitano, dalili zimekuwa kali na matibabu yake yamekuwa na madhara makubwa katika maisha yake.

Alisema: Madaktari wanasema kujaribu hadi mara 18 kuniwekea dawa kwa mshiba, kwa sababu mishiba yangu haipatikani rahisi.

Mara wakifanikiwa kuniwekea dawa, ninaanza kutapika kisha naenda nyumbani.

Chanzo cha picha, Caitlin White

Maelezo ya picha,

Caitlin alitaka awe mwalimu au wakili

"Ninakula nikiwa nyumbani na wakati nikiwa hospitalini.

"Lakini nimepatwa na hali inayojulikana kama septicaemia mara saba kwa mwaka kwa sababu nina kinga mwili ya chini sana."

Hali yake imebadilika kabisa uhusiano wake na marafiki, wengine wakiwa sasa wakiwa wameendelea na maisha yao.

Caitlin anasema: "siwezi kutoka nje kwa chakula au kahawa na marafiki zangu tena kwa sababu nitaaibika sana.

Ninawasiliana nao kupitia Snapchat na Facebook lakini siwaoni sana.

Akiulizwa jinsi hali hiyo imebadilisha maisha yake, Caitlin alisema: Nikiwa mdogo nikilifiki labda ningekuwa mwalimua au labda wakili.

Lakaini wakati nitapata nafuu ningependa kufanya kitu kinacohusu madawa au kusafiri.

Chanzo cha picha, Google

Maelezo ya picha,

Caitlin kwa sasa anapata matibabu katika hospital hii ya Perth Royal Infirmary