Kwa nini si vyema kulala kitanda kimoja na mtoto wako mchanga

mtoto Haki miliki ya picha SOPHIE WHEELER PHOTOGRAPHY/SOLENT
Image caption Mtoto wa wiki sita amekufa kutokana baada ya kulala na mama yake kitanda kimoja

Mama mmoja ametoa onyo kwa akina mama ambao huwa wanalala na watoto wao mara baada ya mtoto wake wa kiume mwenye wiki sita kufa na ripoti ya uchunguzi wa kifo cha mtoto wake kubainisha hivyo pia.

Rowan Leach mwenye umri wa miaka 20, ambaye alikuwa akimlea mtoto wake peke yake alibaini kifo cha mtoto wake mara baada ya kuamka saa sita usiku kumnyonyesha mtoto huyo na kumkuta hapumui.

Mama huyo aliwaelezea wapelelezi wa chanzo cha kifo cha mtoto wake wakati akisubiri huduma ya dharura ikamilike.

"Kifo cha mtoto wangu kimenisikitisha sana"Bi.Leach ambaye alimpoteza mtoto wake Hadley alieleza.

Licha ya kwamba mtoto huyo alikimbizwa hospitalini,wahudumu wa afya walishindwa kuokoa maisha ya mtoto huyo hivyo kufariki majira ya alfajiri mwezi septemba mwaka jana.

Haki miliki ya picha FAMILY/SOLENT
Image caption Rowan Leach akiwa na mtoto wake Hadley wakati wa uhai wake

Bi.Leach kutoka Southampton alikuwa anamlea mtoto wake kwa usaidizi wa mama yake.

Alielezea hali ilivyokuwa kabla ya mtoto wake kufariki,mama huyo anasema alipitiwa na usingizi mara baada ya kumchukua mtoto wake na kumfunika kwa koti lake kwa sababu kulikuwa na baridi kali na lengo lake lilikuwa ni kumnyonyesha baada ya muda.

Huwezi kusikiliza tena
Jane: Nina masponsa wawili na sioni tatizo

"Nilishangaa kumkuta mtoto wangu yuko upande wa pili wakati alikuwa amelala upande mwingin," Bi.Leach alieleza.

Haki miliki ya picha SOPHIE WHEELER PHOTOGRAPHY/SOLEN
Image caption Mazishi ya mtoto Hadley

Mchunguzi mkuu Grahame Short ambaye hakuweza kuelewa kwa haraka chanzo cha kifo cha mtoto huyo kilitokeaje lakini alisema hamlaumu mama huyo kuwa mzembe.

Aliongeza kwa kudai kwamba huwa anawaonea huruma akina mama ambao wanahudumia watoto peke yao bila ya kuwa na wenza wao.

Vilevile uchunguzi uliofanywa haujaleta hali yeyote iliyotiliwa mashaka maelezo ya mama huyo ya namna mtoto wake alivyokufa.

Takwimu zinaonesha kwamba idadi wa watoto 133 wamefariki katika miaka mitano iliyopita kutokana na tabia ya akina mama wanaolala na watoto wao ,kwa mujibu wa data za elimu.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii