Wana anga wajitahidi kuzuia kuvuja hewa kutoka kituo cha kimataifa cha ISS

Two docked Russian spacecraft on the International Space Station (ISS), the Soyuz MS-09 crew ship and the Progress 70 resupply ship

Chanzo cha picha, NASA

Maelezo ya picha,

Chombo cha Urusi cha Soyuz (kushoto) kilileta wana anga kwenye kituo cha (ISS) mwezi Juni

Wana anga kwenye kituo cha kimataifa cha anga za mbali (ISS) wanajaribu kuziba ufa ambao umesababisha hewa kuvuja kutoka kituo hicho kilicho umbali wa kilomita 400 kutoka sayari ya dunia.

Inaamiwa kuwa ufa huo mdogo ulitokea wakati kituo hicho kiligongwa na jiwe dogo lililokuwa likipita kwa kasi ya juu angani

Wanafuatilia kituo hicho huko Texas Marekani na Moscow nchini Urusi, wanasema wanasayansi 6 walio angani hawako kwenye hatari.

Athari za mawe madogo sana ni tisho la kila mara kwa kituo hicho kinachozunguka angani kilichojengwa kustahimili kugongwa na vumbi inayozungika katika anga ya dunia.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mwana anga mjerumani Alexander Gerst atakuwa wa pili kutoka Ulaya kuongoza kituo cha ISS

Wanaofuatia chombo kwanza walijulishwa na mitambo ya kutambua hali hewa iliyo ndani ya chombo hic

Wanasayasi walikuwa wamelala wakati huo, lakini wakati waliamka kuanza siku Jumatano, waliamrishwa kuutafuta ufa huo.

Ufa huo ulipatikana kwenye chombo cha Urusi cha Soyuz kilichotumiwa kusafirisha wana anga tarehe 8 mwezi Juni wakiwemo mwana anga wa Ulaya Alexander Gerst.ho.