Mlipuko mkubwa wa mshambuliaji wa kujitoa mhanga wakumba Mogadishu

Picture showing smoke rising following the blast

Chanzo cha picha, Twitter/@saxafi111

Maelezo ya picha,

Mlipuko mkubwa wa mshambuliaji wa kujitoa mhanga wakumba Mogadishu

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga ameshambulia ofisi ya serikali kwenye mji mkuu wa Somalia, Mogadishu na kusababisha shule iliyokuwa karibu kuporomoka, kwa mujibu wa polisi.

Shambulizi hilo la kutumia gari kwenye wilaya ya Howlwadag liliwaua wanajeshi watatu na kujeruhiwa watu 14 wakiwemo watoto 6.

Mlipuko huo pia uliharibu nyumba zilizo karibu na kung'oa paa la msikiti mmoja.

Kundi la wanamgambo wa al-Shabab ambalo limekuwa likiendesha mashambulizi kwa zaidi ya miaka 10 lilisema liliendesha shambulizi hilo.

Wanajeshi watatu waliuawa walipolisimamisha gari lililokuwa limejazwa milipuko kuingia kwenye makao ya serikali.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Mlipuko mkubwa wa mshambuliaji wa kujitoa mhanga wakumba Mogadishu

Raqiya Mahamed Ali, ambaye alikuwa ndani ya makao hayo alisema: "Tulikuwa tukiendelea na shughuli zetu wakati mlipuko ulitokea.

"Nilijificha chini ya meza. kulikuwa na milio mingi ya risasi kwenye lango...wakati nilitoka nje, niliona watu wengi wakiwa wamejeruhiwa na wengine wakiwa wamekufa." aliiambia Reuters.

Somalia imekumbwa na ghasia tangu mwaka 1991 wakati serikali ya kijeshi ilipinduliwa.

Kupindiuliwa kwa Mohamed Siad Barre kulisababisha miongo kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya wababe wa kivita na sehemu zingine mbili - za Somalilad na Puntland zilijitenga kutoka Somalia.

Sehemu kubwa ya nchi imekuwa kwenye vita.

Chanzo cha picha, Twitter/@abdi_adaani

Maelezo ya picha,

Mlipuko mkubwa wa mshambuliaji wa kujitoa mhanga wakumba Mogadishu