Magari yaliyopata ajali ya kuwatia hofu watu yaletwa mjini Addis Ababa Ethiopia

Magari ya kuwatia hofu watu yaletwa mjini Addis Ababa Ethiopia
Maelezo ya picha,

Magari ya kuwatia hofu watu yaletwa mjini Addis Ababa Ethiopia

Maonyesho ya magari yaliyohusika kwenye ajali za barabarani yameletwa kuonyeshwa kwenye mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Maonyesho hayo yameandaliwa na Samrawit Yirgalem ambaye anasema alinusurika ajali nnne za barabarani.

Magari hayo yametolewa na kampuni za bima nchini humo.

"Ninataka watu wajifunze kutokana na hili," Bi Samrawit aliiambia BBC.

Maelezo ya picha,

Magari yaliyopata ajali ya kuwatia hofu watu yaletwa mjini Addis Ababa Ethiopia

"Mwaka mpya kwenye kalenda ya Ethiopia utakuwa mwezi ujao. Kwa hivyo watu wataamua kuchagua kuwa na mwaka unaokuja usio na ajali."

Shirika la Afya Duniani linasema ajali za barabarani ndio tatizo kuu la kiafya duniani na sasa nchi za kipato cha chini ikiwemo Ethiopia zinaathirika sana.

Wizara ya uchukuzi nchini Ethiopia inasema kuwa watu 4,500 wanauawa kwenye barabara za nchi hiyo kila mwaka na wengine zaidi ya 12,000 wanajeruhiwa kufuatia ajali za barabarani.

Maelezo ya picha,

Magari yaliyopata ajali ya kuwatia hofu watu yaletwa mjini Addis Ababa Ethiopia