Moto wateketeza Makumbusho kongwe ya miaka 200 nchini Brazil

makumusho

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

jengo la Makumbusho hiyo yenye miaka 200

Kikosi cha zimamoto nchini Brazil wanajaribu kuzima moto mkubwa uliotokea katika moja ya makumbusho kubwa na ya kihistoria Mjini Rio De Jeneiro.

Picha za televisheni zinaonesha makumbusho hiyo ikiteketea kwa Moto, Inakadiriwa kuwa na miaka mia mbili na ina mamilioni ya vitu vya historia ikiwemo mifupa ya mwanamke wa kale Zaidi kugunduliwa huko Marekani.

Makumbusho hii inakadiriwa kuwa na vitu milioni 20, haijajulikana bado kama kuna marejuhi yoyote.

Chanzo cha moto bado kinachunguzwa na mamlaka nchini Brazil. Mapema mwaka huu Makumbusho hiyo ilisherekea kutimiza miaka 200.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Rais wa Brazil Michel Temer amesikitishwa na tukio hilo

Rais wa Brazil katika ukurasa wake wa Twitter amasema kuwa, imekua siku ya huzuni kwa wabrazil wote, na kuharibika kwa jengo hilo hakuwezi kufananishwa na thamani ya historia ilioyopotea.

Naye mkurugenzi wa Makumbusho amesema kuwa ni tukio la kusikitisha sana.

Kwa mujibu wa tovuti ya makumbusho, Ndani ya makumbusho kulikua na vitu mbalimbali vya Historia ya Brazil na nchi nyingine ikiwemo Misri.

Sehemu muhimu ya historia iliyopotea katika jengo hilo ni pamoja na mifupa ya watu wa kale ikiwemo mifupa ya mwanamke wa kale kutoka marekani ambaye ina miaka elfu kumi na mbili na mifupa ya waliokua wanyama wakubwa zaidi Duniani maarufu kama dinosaur.

Wafanyaki wa makumbusho hiyo waliwahi kuripoti kutokuwepo kwa bajeti ya kutosha na kusahaulika kwa jengo hilo.