Jinsi wasichana wanavyoathirika na mgogoro Lake Chad.

Ziwa Chad
Maelezo ya picha,

Familia Moja Ziwa Chad

Ripoti mpya imefichua hali mbaya kibinadamu inayoendelea katika eneo la mgogoro la ziwa Chad sasa linawaathiri zaidi wasichana wadogo, Shirika la kutetea haki za watoto la Plan International linasema , vurugu ni sehemu ya maisha ya wasichana katika eneo hilo ambalo lipo kati ya nchi za Nigeria Niger, Chad na Cameroon.

Ikiwa leo Kongamano la siku mbili la kikanda kuhusu ziwa Chad huko Berlin wenye lengo la kuhasisha juhudi za kukabiliana na hali mbaya kibinadamu katika eneo hilo.

Repoti hiyo ambayo imewahusisha wasichana 449 wenye umri wa miaka 10 na 19 ambao waliohojiwa mwezi march na Aprili inasema wasichana hao wamekuwa ni kundi linalonyanyaswa kutokana na jinsia zao pamoja na umri walionao.

Wasichana ambao walihusishwa katika utafiti huo ameelezea jinsi walivyonyanyaswa ikiwa ni pamoja na ukatili wa majumbani. Karibu robo ya wote waliohojiwa wamesema wamewahi kupigwa katika miezi ya hivi karibuni.

Idadi ndogo inayokaribia asilimia nane ya wasichana hao wameeleza waliwahi kushikwa shikwa na kupigwa busu kwa lazima bila ridhaa yao.

Wale waliofanyiwa ukatili wa kingono wamekuwa wakinyanyapaliwa na jamii na kulazimishwa kuolewa na wale waliowafanyia ukatili huo.

Kuna zaidi ya watu milioni mbili walioyakimbia makazi yao katika eneo hilo la ziwa Chad.

Mashirika ya kibinadamu yanakadiria karibu watu milioni 10 wanahitaji msaada wa dharura.

Kongamano hilo la viongozi wa kitaifa inafanyika Birlin unatarajia kukusanya fedha za kuwasaidia waathika, si kwa dharura lakini pia utaweka mikakati ya muda mrefu ya kukabiliana na janga hilo.

Umoja wa mataifa unakadiria karibu dola bilioni 1.6 zinahitajika kukabiliana na hali hiyo mbaya ya kibinadamu.