Damas: Mbuzi maarufu anayefugwa kama mlinzi Njombe Tanzania

Damas: Mbuzi maarufu anayefugwa kama mlinzi Njombe Tanzania

Umewahi kuwaza kumfuga mbuzi awe mlinzi wako? Kama ambavyo wengine hufuga mbwa ama wakati mwingine paka? Mzee Antony Mwandulami mkaazi wa Mkoa wa Njombe Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania anafuga mbuzi kama mlinzi wake. Anasema mbuzi huyo ambaye amefanya kazi kwake kwa miaka 19 sasa humpa taarifa juu ya kila mtu mbaya anayetaka kuja kwake na kumdhuru na ameweza kumnusuru dhidi ya majanga mbalimbali.

Ni kwa namna gani?