Je, huenda nchi za Afrika zikashindwa kulipa madeni ya China?

Chinese workers in Kenya

Chanzo cha picha, AFP

Nchi za Afrika zimeonyesha hamu kubwa kwa mikopo ya China lakini baadhi ya wataalamu sasa wana hofu kuwa bara la Afrika huenda likajikuta kwenye madeni makubwa.

Barabara ya Entebbe-Kampala inaweza kutajwa kuwa kuvutio cha watalii kwa watu nchini Unganda karibu miezi mitatu tangu izinduliwe.

Barabara hiyo ya umbali wa kilomita 51 inayounganisha mji mkuu Kampala kwenda uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebe, ilijengwa na kampuni ya Kichina kwa gharama ya dola milioni 476 kutoka mkopo wa China Exim BANK.

Imepunguza safari ndefu ya saa mbili hadi dakika 45.

Maelezo ya picha,

Mikopo ya China kwa Afrika

Uganda imechukua dola bilioni tatu za mikopo kutoka China katika kile mhadhiri na mwana uchumi mjini Kampala anasema kuwa ni moyo wa kujitolea usio na mpinzani wa kuzipa nchi za Afrika mikopo

Ggoobi anasema kuwa deni la China huchangiwa na biashara kubwa kwa kampuni za China, hasa za ujenzi ambazo zimegeuza bara lote la Afrika kuwa eneo ya ujenzi wa reli, barabara, umeme, mabwawa, viwanja, majengo ya biashara na kadhalika.

Maelezo ya picha,

Barabara mpya kati ya Kampala na uwanja wa Entebbe

Mikopo ya China inakuja wakati nchi nyingi za Afrika kwa mara nyingine ziko kwenye hatari ya kukiuka makubaliano ya kulipa mikopo hiyo.

Chad, Eritrea, Musumbuji, DR Congo, Sudan Kusini na Zimbabwe zinatajwa kuwa nchi zinazokumbwa na tatizo la mikopo mwishoni mwa mwaka 2017 huku viwango vya kukopa vya Zambia na Ethiopia vikishushwa.

Chanzo cha picha, Michael Khateli

Maelezo ya picha,

Mkopo wa China ulifadhili ujenzi wa reli mpya nchini Kenya kutoka Mombasa hadi mji mkuu Nairobi

Mwaka 2017 miradi mipya inayofadhiliwa na China ilikuwa ya thamani ya dola bilioni 76.5.

Hata hivyo mfumo huu wa China una waungaji mkono barani, akiwemo mkuu wa Benki ya Maendeleo Barani Afrika (ADB), Akinwumi Adesina, waziri wa zamani wa kilimo nchini Nigeria.

"Watu wengi hushikwa na hofu kuhusu China lakini mimi sina hofu. Nafikiri China ni rafiki wa Afrika," aliiambia BBC.

Maelezo ya picha,

Vishara kati ya Afrika, EU, China, Marekani na Uingereza

Kwa sasa China ndiyo mfadhili mkubwa zaidi barani Afrika.

Mwaka 2015, utafiti kuhusu China na Afrika uliofanywa na chuo cha John Hopkins, ulionya kuwa huenda nchi za Afrika zinashindwa kulipa madeni ya China.

China inachukua asilimia kubwa ya deni la nchi za Afrika lakini bado zinazidi kukopa kutoka sehemu zingine tofauti, kwa hivyo sio China tu inaweza kulaumiwa kwa deni hilo.

Wakati wa mkutano uliopita mjini Johannesburg, China iliahidi msaada wa dola bilioni 35 kati ya misaada mingine kwa Afrika.

Lakini kulingana na Benki ya Standard, kilichopo sasa ni ukosefu wa biashara na China tangu mwaka 2014. Ni nchi tano tu zilizo na ushirikiano wa kibiashara na China.

Bw Ggoodi anataka China isaidie nchi za Afrika kuwekeza katika sekta tofauti zikiwemo viwanda ili nchi za Afrika zipate kuwa na uwezo wa kuzalisha na kuuza bidhaa nje.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Viongozi wa Afrika hukutana kila mwaka kwenye makao makuu ambayo ujenzi wake ulifadhiliwa na China kwa pauni milioni 2,00 nchini Ethiopia