Wanawake 2 wachapwa hadharani Malaysia kwa kufanya mapenzi ya jinsia moja

An Acehnese woman is lashed by a hooded local government officer during a public caning at a square in Aceh province, on June 12, 2015.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Picha ya maktaba ya mwanamke aliyechapwa Indonesia awali

Wanawake wawili nchini Malaysia waliopatwa na hatia ya kujaribu kufanya mapenzi ya jinsia moja ndani wamechapwa viboko kwenye mahakama ya kidini.

Wanawake hao waislamu wenye umri wa miaka kati ya 22 na 32 kila mmoja alichapwa viboko sita kwenye mahakana ya Sharia katika jimbo la Terengganu.

Kulingana na afisa mmoja ni kuwa hiyo ndiyo hukumu ya kwanza inayohusu mapenzi ya jinsia moja na ndiyo adhabu ya kwanza ya kuchapwa hadharani.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yamekosoa vikali hatua hiyo ya kuchapwa kwa wanawake. Kuchapwa huko kulishuhudiwa na zaidi ya watu 100 kwa mujibu wa vyombo vya habari.

Mwanachama mmoja wa baraza kuu la Terenggau, Satiful Bahri Mamat, alitea adhabu hiyo, akiliambia shirika la Reuters kuwa hatua haikuwa na ya kutesa au kuumiza, na ilifanyika hadhari ili iwe funzo kwa jamii.

Wawili wao ambao majina yao hayakutajwa walimamatwa mwezi Aprili na maafisa wa kulinda itikadi za kiislamu baada ya kupatikana ndani ya gari lililokuwa limeegeshwa eneo la umma huko Terengganu.

Wote walikiri kuvunja sheria za kiislamu na walihukumiwa kuchapwa viboko na faini ya dola 800.

"Vitendo vya kingono kati ya watu wawili wazima havistahili kuchukuliwa kama uhalifu, au kuadhibiwa kwa viboko," shirika linalowahudumia wanawake lilisema.

Kulingana na shirika hilo, kuchapa viboko chini ya sheria za kiislamu haifanani na adhabu ya viboko inayofanywa kwa uhalifu mwingine chini ya sheria za kiraia. Haina lengo la kuzua machungu.