Wanahabari 2 wa Reuters wafungwa miaka saba Myanmar kwa kufanya uchunguzi kuhusu mauaji

Polisi

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Kyaw Soe Oo kushoto na Wa Lone wanadai waliwekewa mtego na polisi

Mahakama ya nchini Myanmar imewahukumu waandishi wa habari wawili wa Reuters kwa kifungo cha miaka saba kwa kosa la kufanya uchunguzi wa siri katika taifa hilo juu ya mgogoro wa Rohingya.

Waandishi hao ambao ni Wa Lone na Kyaw Soe Oo,walishikiliwa kwa kosa la kuwa na nyaraka za serikali ambazo walidai kupewa na askari polisi .Jambo ambalo waandishi hao walidai kwamba lilikuwa limepangwa kimtego.

Kesi hiyo imeonekana kwa wengi kuwa ni uminywaji wa uhuru wa habari nchini humo.

"Sina hofu kwa sababu sijafanya kosa lolote ,nnaamini katika haki,demokrasia na uhuru.wa kujieleza,"Wa lone alisema hivyo baada ya kukamatwa.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mke wake Kyaw Soe Oo(mwanahabari aliyeshikiliwa)

Ni nini kilichokuwa kinachunguzwa?

Waandishi hao walikuwa wanatafuta ushahidi juu ya mauaji ya wanaume kumi yaliyofanywa na jeshi katika kijiji cha Inn Din in huko kaskazini mwa Rakhine mwezi September mwaka 2017.

Waandishi hao walikamatwa kabla ya taarifa yao kuchapishwa ,kwa sababu walikamatwa mara baada ya kupewa nyakara na polisi wawili ambao walikutana nao kwenye mhahawa kwa mara ya kwanza.

Polisi mmoja aliyeshuhudia mpango huo uliopangwa ili kuwakamata waandishi wa habari aliweza kutoa ushuhuda wake.

Ripoti kamili ambayo ilijumuisha waandishi wengine ilioneka kuwa nzuri kwa sababu ilikuwa imekusanya ushaidi kutoka kwa washiriki mbalimbali wakiwa pamoja na wanakijiji ambao walikiri kuwauwa waunini wa kiislamu wa Rohingya na kuchoma nyumba zao.

Wapiganaji wa waasi pia waliwahusisha polisi katika mauaji hayo.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Hawa ni wanaume waliouwawa ambao waandishi hao walikuwa wanachunguza

Jeshi hapo kabla ilizindua ripoti yao ya uchunguzi wakiwashutumu waasi kufanya unyanyasaji huko Rakhine na kujitoa kabisa katika makosa yote.

Serikali badae ilizindua uchunguzi wake juu ya mauaji hayo na kuthibitisha kwamba mauaji hayo ya kimbari yalikuepo na kuhahidi kuwachukulia hatua wale wote waliohusika.

Ni nini kilitokea Rohingya?

Watu takribani laki saba wamehama nchini humo kutokana na mgogoro ambao ulianza mwaka jana.

Mgogoro huo ulizidi kuwa mkubwa mara baada ya kikundi cha wapiganaji wa Rohingya kilipovambia vituo kadhaa vya polisi.

Umoja wa mataifa ilikuwa imelitaka jeshi kutoa majibu ya mauaji,unyanyasaji,ubakaji,Uaibishaji ,utumwa na vitendo vya kikatili uliofanyika kwa vitisho kutoka kwao.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Maandamano ya watu wakitaka waandishi wa habari kuachiwa huru

Balozi wa Uingereza nchini Myanmar alielezea masikitiko yake juu ya kukamatwa kwa waandishi hao wa Reuters.

Huku balozi wa Marekani pia alitoa makosa yanayofanana na ya balozi wa Uingereza na kudai kwamba maamuzi ya mahakama yameumiza kila mtu ambaye amekuwa akitafuta jitihada za uhuru wa habari.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa na mratibu wa haki za kibinadamu huko Myanmar, Knut Ostby, alisema Umoja wa Mataifa "umeomba kuachiliwa huru kwa waandishi wa habari hao .Uhuru wa habari ni muhimili wa amani na haki za binadamu kwa wote. Hivyo uamuzi wa mahakama umewasikitisha sana.

Human rights watch wao pia inafanya jitihada za kuwashawishi wale waliokuwa wamenyamaza kutoa taarifa ya mauji ya askari.

Hukumu hii inaashiria wazi kuwa uhuru wa habari ni mdogo katika serikali hiyo.

Aidha vyombo vya habari vinaonekana kwamba vinamilikiwa na serikali moja kwa moja hivyo ni ngumu kupata taarifa sahihi kutoka nchini humo.