China yaaahidi kuendelea kuisaidia Afrika katika uboreshaji wa maendeleo ya miundo mbinu

China Summit

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Raisi wa China Xi Jinping

Viongozi wa bara la Afrika wameushukuru uamuzi wa China wa kutoa dolla bilioni sitini kwa bara hili kama mikopo, misaada na uwekezaji mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Wakati mkutano mkuwa wa dunia baina ya viongozi kutoka bara la Afrika na China unaofanyika mjini Beijing ukiendelea, China imetamka wazi kuwa italifadhili bara la Afrika dola za kimarekani bilioni sitini ambapo mkutano huo .

Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi ya China hii inajumuisha dola nilioni tano zinalenga kukuza uingizaji bidhaa za Afrika nchini China.

Chini ya mpango huo, China itazindua mpango wa kukuza viwanda na biashara baina ya China-Afrika kama sehemu ya biashara mpya ya dola bilioni 5 mpango wa uwezeshaji ambao una maana ya kurejesha au kupunguza upungufu wa bidhaa za biashara kutoka Afrika kwenda nchini China.

Katika kuimarisha maeneo kumi yaliyotangazwa katika mkutano wa mwaka 2015, tangu mwaka huu uanze , kipaumbele kimewekwa katika maeneo makubwa nane ili kuongeza ushirikiano wa China Afrika na makampuni ya sekta ya binafsi ya Kichina ili kuongeza uwekezaji katika Afrika,katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Kuongezea juu ya hayo nchi ya China imeahidi kuendelea kulisaidia bara la Afrika katika masuala ya uboreshaji wa maendeleo ya miundo mbinu ingawa msisitizo umewekwa katika kulifanya bara hili kusonga mbele katika kuendeleza Soko la Usafiri wa anga wa Afrika moja na kutoa fursa ya safari za anga ya moja kwa moja kati ya China na Afrika.

Kati ya fedha zote, dola bilioni 15 za Marekani zinatengwa kwa misaada, mikopo isiyo ya riba na ya chini ya mikopo, ufafanuzi pia umetolewa juu ya uondolewaji wa dola bilioni kumi za mfuko maalumu wa kuendeleza masuala ya kifedha barani Afrika.