Tahadhari yatolewa kuhusu taarifa potofu za dawa kinga ya minyoo na kichocho Tanzania

  • Esther Namuhisa
  • BBC Swahili
chanjo

Chanzo cha picha, Per-Anders Pettersson

Wataalam wa afya nchini Tanzania wametahadharisha juu ya uwepo wa taarifa katika mitandao ya kijamii zinazoweza kuleta taharuki juu ya dawa kinga dhidi ya minyoo na kichocho zinazotolewa hivi sasa mashuleni nchini humo.

Hii inakuja baada ya kuibuka kwa mijadala kinzani katika mitandao ya kijamii hivi karibuni huku taarifa zisizo na vyanzo vya kuaminika zikinukuu wazazi walio lalamika kwamba watoto wao wamepata "madhara baada ya kupewa dawa hizo na wengime wakilalamikia kutopoewa taarifa ya utoaji wa dawa hizo.

Hata hivyo, mijadala Kama hii juu ya utoaji wa dawa kinga si migeni. Na umekuwa ikihusisha pia utoaji wa chanjo katika nchi mbalimbali na hivyo kuathiri jitihada zinazoanzishwa na serikali na mashirika ya afya Katika kutokomeza magonjwa mbalimbali kama polio.

Nchini Nigeria taarifa za uzushi juu ya chanjo ya polio ziliposambaa mwaka 2003 na kusababisha kampeni hiyo kuwa na ugumu kufanikiwa.

Mgomo huo ambao ulidumu kwa takribani miezi 15 uliweza kusababisha madhara makubwa ya ongezeko la kesi za polio.Ilipofikia mwaka 2008,Nigeria peke yake ilikuwa na maambukizi asilimia themanini na sita ya kesi zote za Polio katika bara la afrika.

Syriacus Buguzi ni daktari kutoka jijini Dar es Salaam, anasema kwamba mjadala wa dawa za chanjo/ dawa za kinga mara nyingi jamii unakuwa na mapokeo tofauti na matakwa ya kisayansi. Nchini Nigeria walikataa chanjo ya polio na kusababisha matokeo hafifu ya malengo ya utoaji chanjo.

Nigeria walipata taharuki ambayo ilisababishwa na kusambazwa habari za uzushi katika mitandao ya kijamii kwamba chanjo hizo zinaweza kusababisha ugonjwa hatari usiojulikana.

Taarifa hiyo ilisababisha taharuki kubwa katika jamii na hata shule zilifungwa baada ya wazazi kukataa kuwapeleka watoto shule wakiogopa chanjo hizo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Chanjo au dawa kinga inapokelewa na mitazamo iliyogawanyika

"Taharuki Kama hizi zilishawahi kutokea Kenya hadi kanisa likawa kwenye mgogoro na serikali na wanasayansi lakini baada ya kuelimishwa, kanisa likabidi kukubali na kutoa elimu kwa jamii...chanjo ikakubalika na taharuki ikabaki historia,"Dr.Buguzi .

Nchini Kenya ,gazeti la Daily Nation liliandika namna ambavyo Kanisa Katoliki lilivyomkosoa kiongozi wa Nasa,Raila Odinga kuhusu chanjo za pepopunda ambazo zilikuwa zinatolewa kwa wanawake wajawazito kuwa na madhara na kuwataka wanasiasa wasijihusishe na masuala ya kisiasa.

Dk.Buguzi amesisitiza pia kwamba kila dawa huwa inategemeana mapokeo ya mwili wa binadamu kama ni hasi ama chanya suala ambalo linatambulika kitaalamu na huwa zina muda wake wa Kuisha na hazimtokei kila mtu au kila mtumiaji.

Maelezo ya picha,

Mwanafunzi akiwa ametoka kwenye chanjo nchini Tanzania

Taharuki hizi zimekuja nchini Tanzania baada ya utoaji wa dawa kinga za minyoo na kichocho kutolewa jana katika shule za binafsi na za Umma kudaiwa katika mitandao ya kijamii kwamba dawa hizo si salama kwa watoto kwa sababu inawapelekea watoto wao kupata madhara ya kiafya.

Licha ya taarifa kutolewa kuhusu utoaji wa dawa hizo na uongozi wa shule kwa njia ya barua ili kuomba ruhusa kwa wazazi kutoa idhini ili watoto wapewe dawa kinga wakiwa shuleni.