WhatsApp: Jambo gani linakukera katika makundi ya WhatsApp uliyopo?

Chanzo cha picha, Getty Images
Makundi ya mitandao ya kijamii ya WhatsApp huwa yanawasilisha umoja wa watu kuwa na malengo yanayofanana.
Lakini hali inakuwa tofauti kwa sababu inaonekana kwamba wengi wanashindwa kufuata kanuni walizojiwekea. Hii inatokea pale ambapo mtu anaingiza maongezi ambayo sio muhimu kwa wakati huo au kuleta ujumbe ambao mahali alipotuma si sahihi.
Je,ni jambo gani ambalo huwa linakukwaza katika makundi ya WhatsApp na namna gani unaweza kuepukana na kero hizo?
Chanzo cha picha, Getty Images
Makundi mengi ya WhatsApp huwa yanatengenezeka haswa wanafunzi wanapokuwa likizo.
Mkuu wa Kundi
Mkuu wa kundi ndio ana mamlaka yote .Hivyo yeye ni muhimu kuweka kanuni zote zitakazoliongoza kundi.
Haitakiwi kuwepo kwa majadiliano baina ya mtu na mtu kwa sababu makundi haya yanajumuisha mawasiliano ya kikundi na sio ya mtu mmoja moja hivyo watu wawili wakiongea masuala yao peke yao kwenye kundi maongezi hayo yanaweza kuwakera wengine.
Kwenye kundi la Whatsapp wana kikundi wanatakiwa kuweka ujumbe ambao unaweza kuwavutia kila mjumbe wa kundi hilo au unaweza kumfurahisha.
Chanzo cha picha, Getty Images
Suala la pili ni kwamba suluhisho ni rahisi ili kuepukana na usumbufu ambao unaweza kuwasababishia watu wengine kwa kumuandikia ujumbe binafsi mtu uliyemlenga na sio kwenye kundi.
Hakikisha kwamba unatuma ujumbe sahihi katika kundi sahihi
Unaweza kuhakikisha mara ya kwanza na ya pili na hata mara ya tatu kabla hujabonyeza kitufe cha kutuma ujumbe.
Kwa sababu usipokuwa makini unaweza kujiaibisha na hata kukupelekea kujitoa kwenye kundi na kuwakwepa watu kwa muda ukifikiria aibu uliyoituma katika kundi la whatsapp.
Usiandike maelezo marefu
Andika maneno kwa ufupi isizidi hata sentensi moja au maneno kumi.
Usiwe mjumbe ambaye huchangii mijadala inayoibuka katika kundi.
Katika makundi ya whattsap hakuna nafasi ya watu ambao hawashiriki katika kuchangia maelezo yoyote pale wanapopokea ujumbe na kuusoma bila kujibu
Hii inaleta ugumu pale ambapo wajumbe wengine kwenye kundi wanasubiri majibu kutoka kwa kila mmoja lakini wengine wanakaa kimya.
Muombe idhini mtu kabla ya kumkaribisha katika kundi
Hivi inawezekana kweli kuwakaribisha watu thelathini katika nyumba yako bila kuwafahamu,kiuhalisia jambo hilo haliwezekani,vivyo hivyo na kwenye makundi ya whatsapp ni lazima watu kuulizwa kama atapenda kujumuika kuwa miongoni mwa wana kikundi.
Na vile vile pale unapoondoka katika kundi ni vyema kusema sababu iliyopelekea ufanye uamuzi huo.